Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kifo hicho kilitokea Septemba 29 mwaka huu saa tano usiku kijijini hapo na kuelezwa kwamba marehemu aliichoma moto nyumba yake huku akiwa ndani.
Ilidaiwa kuwa siku ya tukio marehemu alirudi kutoka matembezini akiwa amelewa huku akipiga kelele na alipofika nyumbani kwake alianza malumbano na mkewe akimtuhumu kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Jacob Mwaluanda alisema wakati ugomvi ukiendelea marehemu alichukua kisu na kumchoma mkewe wake ubavuni na katika harakati za kujiokoa alianguka nje ya nyumba yao na kuzirai hali iliyompa hisia mumewe kwamba ameua ndipo alipoingia ndani na kujifungia kisha kuiwasha moto akiwa ndani yake.
Kutokana na nyumba hiyo kuezekwa kwa nyasi iliwaka moto na kushika kasi haraka ambapo majirani walijaribu kumuokoa bila mafanikio.
Kamanda Mwaluanda alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kubainisha kwamba hali ya mke wa marehemu inaendelea vizuri kwa kuwa alikimbizwa kituo cha afya Mpui muda mfyupi baada ya tukio hilo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment