Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu Moses Kang’ombe
(17) mkazi wa kijiji cha Karundi wilayani Nkasi kuchapwa viboko 20 kutokana na makosa mawili yaliyokuwa
yakimkabili ya kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba
Scolastika Mwanalinze (16) katika shule ya msingi Karundi na kupelekea
kutofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu.
Akitoa hukumu hiyo mbele ya mahakama hiyo hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wiaya Nkasi Ramadhani Rugemalila alisema mahakama
imemkuta na hatia mtuhumiwa baada ya yeye kukiri kutenda kosa hilo na kumtia
hatiani chini ya kifungu cha 130 (1) na
(2)( e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema katika kosa la kwanza la kubaka atachapwa viboko 12
na kosa la pili la kumpa ujauzito mwanafunzi huyo atachapwa viboko 8 na kesi
hiyo haikuhitaji mashahidi baada ya mkosaji mwenyewe kukiri kutenda kosa hilo.
Awali mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Hamimu Gwelo
aliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huu na baada ya
mwanafunzi huyo kukutwa na ujauzito ndipo alipokamatwa na kufikishwa katika
mahakama hiyo na kuwa amevunja sheria chini ya kifungu cha 130 (1) na (2) (e)
na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Aliiomba mahakama hiyo iweze kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa
huyo hasa baada ya vitendo hivyo vya ubakaji na kuwasababishia ujauzito
wanafunzi ili liwe ni fundisho na kwa wengine wenye nia ya kufanya vitendo
hivyo haramu
Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo kwa kuzingatia kuwa
mtuhumiwa huyo alikua chini ya umri wa miaka 18
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment