Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Afya Dk. Seif Rashid amesema huduma za afya hapa nchini zimekuwa zikidorora
kutokana na baadhi ya wahudumu wa afya kutumia vibaya vifaa tiba vilivyopo
kwenye maeneo yao ya kazi.
Waziri
huyo wa afya ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua kituo cha
upasuaji cha Mtowisa kilichopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ambacho
kimejengwa na mashirika matatu ya kimataifa yaliyoungana katika kutoa huduma ya
afya Uzazi na Mwana.
Akizungumza
na wananchi wa tarafa hiyo Dk. Rashid amesema pamoja na serikali kujitahidi
kuboresha huduma za afya hapa nchini bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto
nyingi za kiutendaji na bajeti ya kutosha.
Amesema
wahudumu wa afya wanatakiwa kuwa waadilifu katika vituo vyao vya kazi kwani
wapo baadhi yao ambao hata vifaa tiba vinavyotolewa kwenye maeneo yao wamekuwa
wanavitumia ovyo na kuhariribika kwa haraka lakini baadhi pia wamekuwa
wakituhumiwa kuvihamisha vifaa hivyo na kupeleka kwenye sehemu sizizo kusudiwa
hivyo kufifisha mikakati ya serikali ya kuiboresha huduma za afya.
Amewataka
wahudumu wa afya kutumia muda wao na taaluma walizonazo katika kutoa huduma
zilizobora kwa wananchi kama yalivyo malengo ya serikali katika kutoa huduma
bora za afya.
Aidha
Dk. Rashid ameyapongeza mashirika ya Africare, Plan International na Jphgo kwa
ushirikiano wao kwa kuhakikisha huduma za afya kwa akinamama wajawazito na
watoto wachanga zinapatikana katika mkoa wa Rukwa, kwa kuamua kujenga vya
upasuaji vya Mtowisa wilayani Sumbawanga na Wampembe wilayani Nkasi.
Amesema
maeneo hayo na mengineyo nchini yamekuwa tatizo la upatikanaji kwa huduma za
haraka za upasuaji hivyo kupoteza uhai wa wanawake na watoto wengi.
Mkurugenzi
wa Afya ya Uzazi na Mwana Gwynneth Wong amesema shirika hilo linajitahidi
kuweka mikakati ya kupunguza baadhi ya changamoto katika maeneo ya mradi huo
ikiwa ni pamoja kujenga vituo vya upasuaji sanjari na kutoa magari ya wagonjwa
ili kuokoa uhai wa akinamama wajazito na watoto wachanga.
0 comments:
Post a Comment