Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Rukwa, imewahukumu watu wanane
wa Kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga, kutumikia kifungo cha miaka
56 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuteketeza mali za mwekezaji
zenye thamani ya zaidi ya Sh 227 milioni.
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Adamu Mwanjokolo, alisema washtakiwa walitenda kosa hilo Oktoba 12 mwaka jana.
Alisema uhalifu huo waliufanya katika kambi ya
mwekezaji ambaye ni Efatha Ministry iliyoko Kijiji cha Ulinji ndani ya
shamba la Dafco Malonje linalomilikiwa na mwekezaji huyo.
Hakimu Mwanjokolo alisema washtakiwa wamehukumiwa kwenda jela miaka saba kila mmoja.
Aliwataja watu hao kuwa ni Alexander Kisanko,
Julius Kazembe, Paul Kazikulima na wenzao watano ambao waliruka dhamana
wakati kesi ikiwa mahakamani.
Mwanjokolo alisema ushahidi wa mashahidi sita
umethibitisha kwamba watuhumiwa kwa pamoja walivamia kambi hiyo na
kuchoma moto matrekta mawili na magunia 188 ya mahindi.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment