MATUKIO ya mauaji ya kikatili yanayosababishwa na imani za
kishirikina mkoani Rukwa yamepungua hadi kufikia matukio 30 kwa
kipindi cha mwaka jana ukilinganisha na matukio 37 yaliyoripotiwa
mwaka 2012.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa , Jacob
Mwaruanda, alisema kuwa kupungua kwa mauaji hayo kunatokana na
ushirikiano wa jeshi hilo na wadau wa ulinzi.
Alisema kuwa miongoni mwa makosa ya jinai yaliyogusa hisia za
watu wengi ni pamoja na matukio ya watu wenye ulemavu wa ngozi
‘albino’ waliovamiwa kwa nyakati tofauti na kukatwa mkono mmoja kila
mmoja.
“Pia matukio ya wanavijiji wanaozunguka mashamba ya Shirika la
Ephata wilayani Sumbawanga kuvamia mashamba hayo na kuwapiga walinzi,
kuharibu mazao na kuteketeza matrekta kutokana na mgogoro wa ardhi
kati yao,” alibainisha.
Alisema kuwa watuhumiwa wa matukio hayo walikamatwa na mashauri
yao yapo katika hatua mbalimbali za kutolewa uamuzi mahakamani.
Chanzo;tanzania daima
0 comments:
Post a Comment