Home » » FAMILIA SUMBAWANGA YAZUA KIOJA KORTINI

FAMILIA SUMBAWANGA YAZUA KIOJA KORTINI

Sumbawanga. Mahakama ya Mwanzo mjini Sumbawanga mkoani Rukwa jana iligeuka uwanja wa mapambano kati ya Polisi wa Kituo Kikuu na familia ya Mzee Anastazio Sikombe (62) baada ya familia hiyo kuanza kuwashambulia polisi waliokuwa wakitaka kuwakamatwa kwa tuhuma za kuingia na kulima katika shamba la mtu mwingine kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Polisi Mkoa wa Rukwa, tukio hilo lilitokea saa nne asubuhi ikiwa ni muda mfupi tangu mzee huyo akiwa na familia yake ya watoto watano wawasili katika viwanja vya mahakama hiyo kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa shauri jingine ndipo polisi mmoja alipotaka kuwakamata kwa madai walilima kwenye shamba la Ernest Mwanisenga (49) kinyume na sheria.
Taarifa zinaeleza kuwa polisi huyo alipojaribu kuwatia nguvuni familia hiyo ikiongozwa na mzee huyo walianza kumshushia kipigo polisi huyo, lakini ghafla polisi wengine wapatao sita walijitokeza na kuanza kumsaidia mwenzao kwa kupambana na familia hiyo, sakata ambalo lilidumu kwa zaidi ya dakika saba hadi kumi na kuwafanya watu kutoka katika vyumba vya mahakama ambako mashauri yalikuwa yakiendelea na kwenda kushangaa tukio hilo.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa mapambano hayo kati ya familia hiyo na polisi yalikuwa makali kwani wanafamilia hao walikuwa wakijihami kwa kutumia silaha za jadi kama fimbo na marungu, lakini walidhibitiwa na polisi hao kiasi cha mwenzao mmoja kuzimia kwa dakika kadhaa ambapo muda mfupi baadaye gari yao aina ya Defender lilifika na kuwachukua watuhumiwa hao na kuwafikisha kituo cha polisi
Chanzo:Mwananchi
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa