Sumbawanga. Mvua kubwa iliyonyesha juzi katika
Kijiji cha Kasense, imesababisha hasara ya Sh88 milioni, baada ya
kuharibu nyumba mbalimbali zikiwamo za wanakijiji, taasisi na nyumba za
ibada, likiwapo Kanisa Katoliki.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani
Rukwa, Kassimu Sengusa alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti
hili aliyetaka kujua tathmini ya hasara iliyowapata wananchi baada ya
mvua hiyo kunyesha.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema baada ya timu ya
wataalamu wa manispaa hiyo kufika eneo la tukio na kufanya tathmini
walibaini hasara iliyopatikana ni Sh88 milioni, na kwamba nvua hiyo
iliyoambatana na upepo mkali iling’oa paa za nyumba za watu 28, na
nyumba mbili za waganga wa zahanati ya kijiji hicho.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment