Home » » Hofu ya uti wa mgongo yatanda gerezani Rukwa

Hofu ya uti wa mgongo yatanda gerezani Rukwa

HOFU na shaka vimetanda kwa watendaji wa idara ya magereza mkoani Rukwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo mkoani humo. Tayari watu watano wamekwisha kufariki dunia huku zaidi ya 20 wameugua ugonjwa huo.

Hofu hiyo ilijitokeza jana katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa wilaya, watendaji wa serikali, madaktari na viongozi wa dini.

Kikao hicho kilijadili mbinu mbalimbali zitakazotumika kukabili ugonjwa huo katika Wilaya za Sumbawanga mjini na vijijini, maeneo ambayo ndipo kunakodaiwa wagonjwa wanatoka.

Kamishna Msaidizi wa Gereza la Mahabusu Sumbawanga mjini, Job Lusesy alisema katika gereza hilo hali ni mbaya kwa vile linakabiliwa na mrundikano wa wafungwa.

Alisema jitihada za makusudi zisipochukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwahamisha baadhi ya wafungwa kuwapeleka katika Gereza la Mollo ambalo ni kubwa, huenda mlipo wa ugonjwa huo ukatokea katika gereza hilo.

Nao viongozi wa dini walikubaliana kuwa iwapo hali hii itaendelea watalazimika ibada ziwe zinafanyika nje ya makanisa ikizingatiwa baadhi ya makanisa ni madogo na hayana madirisha ya kutosha hivyo kuleta hofu ya kusambaa kwa homa ya uti wa mgongo kwa waumini wao. 

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga, Makori Mussa aliwaasa waganga wa jadi mjini humo kuacha tabia ya kuwashikilia wagonjwa kwa vile wanawachelewesha kufika hospitali kuanza kupewa tiba.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka aliwaasa viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanafuata maelekezo ya wataalamu wa afya.

Alisema wakiona hali inazidi kuwa mbaya hata baadhi ya shughuli za jamii zinazohusisha mikusanyiko ya watu ipigwe marufuku hadi ugonjwa huo utakapokwisha.
Chanzo: Rai

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa