Home » » WATAKA DINI ITAMBULIWE KAMA MHIMILI WA DOLA

WATAKA DINI ITAMBULIWE KAMA MHIMILI WA DOLA


Mussa Mwangoka, Nkasi.

BAADHI ya wakazi wa kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa wametaka katiba mpya ijayo itambue dini kuwa ni sehemu ya muhimili wa dola.

Mmoja wa wakazi hao, Hassan Mustapha alisema jana wakati akitoa maoni yake mbele ya tume ya kukusanya maoni kundi la mkoa wa Rukwa, iliyotembelea kata hiyo na kufanya mkutano wa hadhara wa kukusanya maoni hao.

Alisema kuwa viongozi wa dini wamekuwa kimbilio la viongozi wa Serikali katika kuomba mchango wa mawazo juu ya uendeshaji wa nchi,kufanya maamuzi magumu hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa viongozi wa dini ipo haja sasa watambulike kwenye katiba ijayo na dini iwe muhimili wa nne wa nchi.

Alisema kuwa  Katiba isiishie kuwatambua tu viongozi hao lakini wawe na wizara yao ambayo itashugulikia masuala mbalimbali yanayohusu dini pasipo kuingiliwa katika utendaji wake.

“alisema kuwa kama ambavyo waandishi wa habari wanataka kutambuliwa kuwa  sehemu ya muhimili wa nchi basi sasa na viongozi wa dini watambuliwe kwenye katiba hiyo ijayo, wana nafasi kubwa katika kusaidia maendeleo ya nchi” alisema Mustapha.

Aliongeza kuwa katiba hiyo pia iweke mgawanyo sawa wa madaraka miongoni mwa watumishi wa Serikali kwa kuzingatia dini zote.

Naye Iddy Ally alipendekeza katiba hiyo kuitambue mahakama ya kadhi na umoja wa nchi za kiislamu (OIC) kwa kuwa  havina madhara yoyote kwa nchi.

Hata hivyo alidai kuwa vyombo hivyo viwekewe utaratibu wake pasipo kuingiliwa huku vikiwa na kanuni zake zinazoheshimika.

Alipoulizwa na mjumbe wa tume hiyo Richard Lyimo iwapo anafahamu maana ya OIC hakuweza kufafanua lolote zaidi ya kueleza kuwa si jukumu la mjumbe huyo kumuuliza swali badala yake anapaswa kuchukua maoni yake.

Awali akitoa maelezo kuhusu utoaji wa maoni ya Katiba mpya ijayo, Mwenyekiti wa tume hiyo kundi la mkoa wa Rukwa, Ester Mkwizu alisema kuwa wananchi wanapaswa kutoa maoni yao bila woga kwa kuwa ipo sheria inayowalinda kufanya hivyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa