Na Sammy Jumaa Kisika, Rukwa.
Mahakama ya hakimu mkazi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, imemhukumu mkazi wa kijiji cha Katazi wilayani humo Geradi Choma (37) ,adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mwanae wa kambo mwenye umri wa miaka tisa.
Adhabu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo Mh. Adamu Mwanjokolo, baada ya Geradi kukiri mahakamani hapo kuwa alitenda kosa hilo Julai 7 mwaka huu majira ya saa sita usiku wakati mkewe akiwa safarini mjini Sumbawanga.
Mwendesha mashtaka toka jeshi la polisi Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Shani katika ushahidi wake, amesema kuwa siku hiyo usiku baada ya Geradi kurejea kutoka kwenye matembezi yake alimkuta binti huyo akiwa amelala chumbani na watoto wenzake, lakini alimwamsha na kumpeleka kwenye chumba cha wazazi wake kisha kumbaka na kumtishia kuwa atamroga iwapo angelimwambia mtu yeyote kuhusiana na kitendo alichofanyiwa.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mwanjokolo amesema kitendo alichofanya Geradi ni cha hatari na aibu hivyo anastahili adhabu hiyo, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye kufanya vitendo kama hivyo.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment