Home » » SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ILIVYOFANA MKOANI RUKWA JANA

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ILIVYOFANA MKOANI RUKWA JANA


 Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa nasaha zake kwa timu
zote mbili kabla ya kipindi cha pili baada ya mapumziko kuanza.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi na
watumishi wa Mkoa wa Rukwa katika uwanja wa Nelson Mandela jana wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi.

Wafanyakazi
wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wakionyesha mafunzo ya mfano kwa
vitendo kwa mgonjwa wa Fistula katika sherehe za Meimosi zilizofanyika
jana katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa ambapo mgeni rasmi
alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Ujumbe uliobeba
onyesho hilo ni kwamba ugonjwa wa Fistula unatibika na wagonjwa
wanashauriwa kwenda katika vituo vya afya waweze kupata tiba. Kitaifa
sherehe hizo zilifanyika Mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais
Jakaya Mrisho Kikwete.
TTCL wakifanya onyesho lao la ufundi na utoaji huduma mkaoni Rukwa
Zimamoto wakifanya onyesho la kuzima moto
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiingia kwa maandamano katika uwanja wa Nelson Mandela.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa na viongozi mbalimbali
wa vyama vya wafanyakazi wakisubiri kupokea maandamano ya wafanyakazi
katika uwanja wa Nelson Mandela katika Manispaa ya Sumbawanga jana
kwenye sherehe ya Siku ya Wafanyakazi duniani. Mgeni Rasmi wa Sherehe
hiyo alikuwa Mkuu huyo wa Mkoa, Kitaifa sherehe hiyo imefanyika Mkoani
Tanga ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi. Kaulimbiu ya
sherehe hiyo mwaka huu ni "Mishahara duni, Kodi kubwa na Mfumuko wa bei
Pigo kwa wafanyakazi"

Picha kwa Hisani ya Full Shangwe Blog

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa