Home » » Wanasiasa Rukwa kikwazo cha CHF.‏

Wanasiasa Rukwa kikwazo cha CHF.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Walter Mguluchuma


Sumbawanga.

BAADHI ya wanasiasa mkoani Rukwa wametajwa kuwa ni sehemu ya kikwazo cha kutofanikiwa kwa mfuko wa afya ya jamii (CHF)kutokana na  kile kinachodaiwa kuwakataza wananchi kuchangia gharama za kujiunga mfuko huo.

Mratibu wa mfuko wa bima ya afya mkoa, Abriel Mkaro alisema hayo wakati akitoa mada katika kikao kilichokuwa na lengo la kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya wajawazito, sambamba na kuhimiza jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kilichowashirikisha wadau wa mfuko huo na kufanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga mjini hapa.

Mkaro alisema kuwa baadhi ya madiwani wamekuwa wakiingilia zoezi la CHF kwa kukataza wananchi wasitoe mchango wa Sh 10,000 kwa kisingizo kwamba ni gharama kubwa na hawezi kumudu kutokana na kukabiliwa na umasikini wa kipato.

Aliongeza kuwa hali hiyo imesababisha wananchi wengi vijiji wasiwe na mwamko wa kujiunga na mfuko huo hivyo kujikuta wakiendelea kupata matibabu kwa gharama kubwa na wengine wakishindwa kabisa kumudu gharama hizo.

Alishauri wanasiasa kuachana na tabia hiyo kwani uchumi wa wananchi wengi kwa mikoa wa Rukwa na Katavi unawapa fursa ya kujiunga na mfuko huo ambao unawawezesha kupata matibabu kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alitaka kamati za afya za halmashauri za wilaya ziweke usimamizi mzuri wa vifaa tiba na dawa zinazofikishwa kwenye zahanati na vituo vya afya ili ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa hali ambayo itapunguza kero kwa wananchi ya ukosefu wa dawa.

Manyanya alisema kuwa kukosekana kwa dawa katika vituo hivyo imechangia wananchi kutohamasika kujiunga na CHF hivyo ili kutatua changanoto hiyo kamati hizo zinatakiwa kubadilika na kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia dawa hizo.

Takwimu zinaonyesha kwamba kimkoa idadi ya kaya zilizojiunga na CHF ni 3,450 kati ya kaya 199,766 sawa na asilimia 1.72 wakati malengo ya kitaifa kufikia 2015 ni asilimia 
30.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa