RUKWA KUPATA UMEME WA UHAKIKA : JIWE LA MSINGI LAWEKWA KATIKA MRADI MKUBWA

Na Khadija Dalasia
Mkoa wa Rukwa unatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dr.Dotto Mashaka Biteko, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia ambao utaunganisha Bara la Afrika kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi mradi huo wa TAZA iliyofanyika leo, Julai 29, 2024, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Kata ya Malangali, Mheshimiwa Dr. Biteko amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia takribani shilingi bilioni 15 kila Mwaka kununua umeme kutoka nchi jirani ya Zambia kwa ajili ya kuhudumia Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu amebainisha kuwa hatua ya kuunganishwa kwa Mkoa wa Rukwa katika gridi ya Taifa itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vya kuchakata na kusindika mazao hasa kwa kuwa Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo.

Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu ametoa maagizo kwa Mkandarasi wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) kuhakikisha kuwa umeme unawashwa katika vijiji 30 ambavyo bado havijafikiwa ifikapo Agosti 30, 2024.

 

KAMATI YA SIASA YA MKOA WA RUKWA YATAKA USIMAMIZI MADHUBUTI MIRADI YA UJENZI.

Na Khadija Dalasia

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa ikiongozwa na Mheshimiwa
Mwenyekti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa, Hajjat Silafu Jumbe Maufi imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Rukwa kusimamia vyema miradi ya ujenzi katika maeneo yao.

Kamati hiyo imegiza hayo leo Julai 25, 2024 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa amesema kuwa ili kupata miradi yenye ubora unaolingana na thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali, Wakurugenzi wanatakiwa kuisimamia kwa karibu ikiwemo kuwawezesha wahandisi kuisimamia kwa karibu.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere amesema amepokea  maelekezo  ya Chama cha Mapinduzi na kuahidi kuhakikisha Wakurugenzi wanatekeleza maagizo hayo.

Kamati ya Siasa imekagua miradi  6 yenye thamani ya shilingi Bilioni 23.6  katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kalumbaleza , ukamilishaji wa vyumba 4 vya madarasa Shule ya Sekondari  Mazoka, ukarabati wa barabara ya Ntenzo – Muze – Kilyamatundu, ukamilishaji wa vyumba 4 vya Madarasa Shule ya Sekondari Zimba, Ununuzi wa Boti 2 za doria katika Ziwa Rukwa na ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Ilemba.




CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA

Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa ikiongozwa na Hajjat Silafu Jumbe Maufi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa imeridhishwa na ubora wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa imeanza ziara ya siku nne katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa ikikagua  utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 -2025 katika Mkoa wa Rukwa kuanzia tarehe 24 Julai hadi tarehe 27 Julai 2024.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa wamekagua utekelezaji wa miradi  8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Miradi iliyokaguliwa ni  ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Senga, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Wipanga, ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Sumbawanga Asilia.

Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa Wodi  Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga - Isofu, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mazoezi Kata ya Chanji, ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Sokolo Kata ya Kizwite , ujenzi wa  vyumba vya madarasa sita na matundu nane  ya vyoo katika Shule ya Sekondari Lwiche na ujenzi wa Vyumba tisa vya Madarasa  na matundu vyoo 8  katika Shule ya Sekondari Kizwite.

Kamati imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuweka katika mipango na bajeti fedha kwa ajili ya kuzijengea uzio Shule zote ili kuimarisha ulinzi  kwa wanafunzi  na kuzuia uvamizi wa maeneo ya Taasisi za umma.



WAKULIMA NKASI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA UMWAGILIAJI KUINUA KIPATO.



Na Khadija Dalasia,
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi  wa Kata za Kirando, Kipili na Kitete Wilayani Nkasi kutumia fursa ya mradi wa umwagiliaji unaojengwa katika Kata hizo kuinua kipato chao.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Julai 23, 2024 aliposhuhudia utiaji saini na makabidhiano ya mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Lwafi - Katongolo kati ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Mkandarasi M/S Halem Construction Company Limited. Zoezi la makabidhiano ya mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 20.9 utakaotekelezwa kuanzia Julai 2024 hadi Julai 2026 limefanyika katika Kijiji cha Katongolo wilayani humo.

Mheshimiwa Makongoro amewaeleza wananchi kuwa lengo la Serikali ni kuwawezesha wakulima kufanya shughuli za kilimo muda wote wa mwaka pasipo kutegemea msimu wa mvua pekee.


Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka  wananchi wa Kata hizo kulinda miundombinu ya mradi ili uwe na manufaa kwa jamii kama ilivyokusudiwa na Serikali huku akimtaka Mkandarasi kuhakikisha anajenga na kutekeleza mradi kwa ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha.


Matukio mbalimbali kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga Mkoani Rukwa

Matukio mbalimbali kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga Mkoani Rukwa


Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa kwenye hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Kianda Mkoani Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kianda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Kampasi ya Rukwa kuhusu ujenzi wa Kampasi hiyo tarehe 17 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa kwenye hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Kianda Mkoani Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.

Taswira ya Majengo ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la Msingi ujenzi wake tarehe 17 Julai, 2024.

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wananchi wa Laela Mkoani Rukwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Laela mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Rukwa tarehe 17 Julai, 2024

Shamrashamra za Wananchi wa Laela wakati wakimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.
 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa