Home » » RC RUKWA AZUIA TANI 2143 ZA MADINI KUUZWA NJE YA NCHI

RC RUKWA AZUIA TANI 2143 ZA MADINI KUUZWA NJE YA NCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.




Katika kasi ya kuhakikisha madini ya watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.

Sakata hilo liliibuka baada ya Mh. Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.

Usafirishaji wa madini hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.

Wakati Mh. Zelote akiendelea na ukaguzi katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.

“Sisi tunajuwa kwamba bandari hii inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, Haiwezekani tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials” kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na sio “raw materilas.” Mh. Zelote alisema.

Na kuongeza kuwa Utaratibu uliopo ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe. 

Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.

Kwa upande wake afisa wa bandari hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa