Home » » MBINU MPYA ZA WIZI ZALIZA DODOMA

MBINU MPYA ZA WIZI ZALIZA DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amechukizwa na kitendo cha Hospitali Teule ya Wilaya ya Namanyere (NDDH), kwa kushindwa kufuata kanuni za mkataba uliopo kati yao na serikali na kuitaka Halmashauri ya Wilaya Nkasi 
kupitia madiwani kuchukua hatua ikiwa hari hiyo itaendelea. Akizungumza jana, baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Rukwa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Boniface Kasululu, alisema amepata taarifa za kiutendaji zisizoridhisha za hospitali kukiuka mikataba waliyowekeana na serikali, kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Alisema serikali inapeleka fedha nyingi katika hospitali hiyo sambamba na watumishi kadhaa wa serikali, lakini taarifa alizonazo zimemvunja moyo na kuwapa jukumu madiwani kufuatilia ikiwamo kuchukua hatua.

Waziri Ummy alifafanua kwa sasa mikataba yote ya namna hiyo, itakuwa inafanywa na madiwani, ili wawe na uwezo wa kuchukua hatua stahiki pale mambo yanapokwenda kinyume cha mkataba waliowekeana. Aidha, Ummy alizitaka halmashauri zote mkoani Rukwa kujenga hospitali zao za wilaya kwa kuwa ndio mpango wa sasa na hilo ndilo litakuwa suluhisho la changamoto wanazokumbana nazo kwenye mikataba ya ubia na hospitali za mashirika.

“Serikali ni lazima iwe na hospitali zake na hizi za mashirika zitatumika pale itakapoonekana kuna uhitaji kulingana na eneo husika na idadi ya watu, lakini sasa hospitali za serikali ni lazima ziwepo na hili ni lazima likamilike haraka sana,” alisema Ummy. Katika hatua nyingine, Waziri huyo aliupongeza Mkoa wa Rukwa kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 95 na wajawazito wengi kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma. Alisema mpango wa serikali sasa ni kutaka kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia kubwa na Mkoa wa Rukwa umeonyesha njia ya kufanikiwa na licha ya kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa afya, lakini wamefanikiwa katika hilo.
Kutokana na jitihada hizo, Ummy aliuahidi mkoa huo, kuwa katika ajira mpya watahakikisha wengi wa watumishi hao wanapelekwa huko, ili kurahisisha huduma hizo kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Ummy, serikali imejipanga kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi zaidi na imepanga kujenga vituo vya afya vitatu kwa kila wilaya na kwa nchi nzima zitajengwa zahanati 500.

Waziri Ummy amemaliza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa ambapo alikagua shughuli mbalimbali za afya.
Imeandikwa na Gurian Adolf na Ibrahim Yassin (Nkasi).
Chanzo:Nipashe
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa