Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mh.
Zelote Stephen (mwenye miwani) akioneshwa kitanda cha kujifungulia na
RMO Dk. Boniface Kasululu muda mfupi kabla ya kuvikabidhi kwa Wakuu wa
Wilaya. kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura
akifuatiwa na Katibu tawala wa Mkoa Bernard Makali.
Katika
kuendeleza dhana ya maendeleo hayana chama Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewashirikisha madiwani wa chama cha
CHADEMA katika harambee ya ghafla iliyolenga kumalizia ujenzi wa jengo
la huduma za afya ya uzazi na mtoto katika kituo cha afya Mazwi,
Manispaa ya Sumbawanga.
Harambee
hiyo ilifanyika muda mfupi kabla ya Mh. Zelote Kukabidhi jumla ya
vitanda vya kujifungulia 16, vitanda vya wagonjwa 80, magodoro 80 pamoja
na mashuka 200 kwa wakuu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya mgawo wa vifaa
hivyo uliofanyika nchi nzima kupitia juhudi za Rais Dk. John Pombe
Magufuli katika kuimarisha huduma za uzazi nchini.
Akiongea
mbele ya wananchi waliohudhuria katika tukio hilo Mh. Zelote alisema
kuwa serikali ya awamu ya tano sio ya maongezi bali vitendo hivyo
kuwataka waheshimiwa madiwani sita wakiwemo watatu wa CHADEMA
wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Sumbawanga kuchangia ujenzi wa jengo
hilo jipya ili kuboresha huduma kwa wananchi waliowachagua.
“Ili
Manispaa iwe jiji tunahitaji huduma bora katika kituo hiki hivyo basi,
Mimi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen nachangia tani tano za
“cement” ambayo ni mifuko 100,” alitangulia kusema.
Harambee
hiyo ilikusanya ahadi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 5.5
huku jengo hilo likiwa limegharimu Shilingi Milioni 16 hadi kusimama.
Awali
akisomewa taarifa kabla ya kuzindua huduma ya kujifungua iliyoanza
tarehe 1/7/2017 katika kituo hicho afisa muuguzi Mariam Kidya alieleza
kuwa jengo lililopo la huduma ya afya ya uzazi na mtoto lina uwezo wa
kuhudumia kina mama 2,327 lakini kwa mwaka 2016/2017 limeweza kuhudumia
kina mama 31,257 jambo lililopelekea kuanzisha ujenzi wa jengo jipya ili
kuimarisha utoaji wa huduma kwa akina mama.
Aidha
Mh. Zelote aliwasisitiza wananchi kuendelea kulipa kodi ili kuendelea
kuboresha huduma na kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini na
kuonya kuwa wale watakaolipishwa ili kupata huduma ya afya ya uzazi na
mtoto basi wafike ofisini kwake ili achukue hatua.
“Ndio
maana Mheshimiwa Rais amesisitiza sana watu tulipe kodi wote ili
kutatua kero mbalimbali za wananchi hususan watu wa hali ya chini.
Nataka nisisitize ulipaji wa kodi ili kazi kama hii na zingine
zifanyike.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa mkoa Dk. Boniface kasululu alipokuwa akisoma
taarifa ya huduma ya afya na uzazi ya mkoa, alisifu uamuzi wa Rais Dk.
John Pombe Magufuli wa kununua vifaa hivyo kupitia bohari kuu ya dawa
(MSD) kwani changamoto hizo zimekuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu kuanzia
ngazi ya mkoa hadi katika halmashauri.
“Sekta
ya afya kukabiliwa na changamoto kadhaa kubwa ikiwa ni upungufu wa
vifaa na vifaa tiba muhimu na ufinyu wa miundombinu ya kutolea huduma
kwa maana ya majengo, hivyo tunapongeza juhudi za rais wetu mpendwa
kutupatia vifaa hivi na tunaahidi kuvitunza ili viweze kuwasaidia kina
mama wa mkoa wetu,” Alisema.
0 comments:
Post a Comment