Home » » MUME AUA MKE AKIDAIWA KUHONGA KODI YA MAJENGO

MUME AUA MKE AKIDAIWA KUHONGA KODI YA MAJENGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Imeandikwa na Pety Siyame, Sumbawanga
 


WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti katika mkoa wa Rukwa, akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mafulala Manispaa ya Sumbawanga, Anna Kashamsakula (35) aliyeuawa kikatili baada ya kuchinjwa na mumewe, baada ya kumtuhumu kumhonga mwanamke mwingine Sh 30,000.
Mshtakiwa alipewa fedha hizo na mkewe ili akalipe kodi ya jengo, waliyokuwa wakidaiwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa. Akithibitisha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema kuwa mauaji hayo yalitokea Julai 27, mwaka huu saa sita usiku katika kijiji chaMafulala.
Akifafanua, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, ambapo marehemu alimpatia mumewe Sh 30,000 ili akalipie kodi ya jengo, ambapo hakulipa bali alienda kutumia na mwanamke mwingine.
Inadaiwa kuwa mume huyo alipewa kiasi hicho cha fedha na mkewe Julai 25, mwaka huu, lakini hakurudi hadi siku iliyofuata, ambapo ugomvi wa maneno uliibuka miongoni mwao hadi Julai 27, mwaka huu mume huyo alipoamua kumuua mkewe na kutokomea kusikojulikana.
CHANZO HABARI LEO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa