Home » » JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME.

JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



 Na Walter Nguruchuma- Katavi yetu
MAHAKAMA ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa  imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Mashete , Titho Solwe (20)  kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10.

Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo ya Wilaya , Lilian Lutehangwa alisema kuwa mahakama  imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo  na upande wa mashtaka pasipo kutia shaka yeyote kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo  na walasi si mtu mwingine .

Upande wa Mashtaka ulioongozwa na Mwendesha Mashataka , Mkaguzi wa Polisi , Hamimu Gwelo  uliita mashahidi watatu mahakamani  hapo . “Mahakama hii  imeridhishwa na ushahidi uliotolewa  na upande wmashtaka ambao hauachi chembe  yayote ya mashaka kuwa  si mtu mwingine aliyemtendea unyama  mtoto  huyo bali ni huyu mshtakiwa  mwenyewe” alisema akitoa hukumu hiyo .

Awali Gwelo alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda uhalifu huo Juni, 19 mwaka huu  katika kijiji cha Mashete kilichopo katika Kata ya Mtenga  wilayani Nkasi  mkoani hapa .
 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa