Na. JOVINA BUJULU – MAELEZO
11/01/2017
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imefanikiwa kukamilisha mkakati wa kitaifa wa magonjwa yasiyo ya
kuambukiza wa mwaka 2013-2020.
Hayo
yamesemwa jiji Dar es salaam na Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukizwa
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Profesa Ayoub Magimba.
Profesa
Magimba amesema kuwa mkakati huo ni muendelezo wa utekelezaji wa
maazimio ya vikao vya 66 na 68 vya Umoja wa Mataifa vilivyofanyika mwaka
2015 na 2016 ambapo Tanzania iliridhia kupambana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza.
“Katika
kuimarisha huduma za kinga kwa magonjwa hayo, Serikali inatoa elimu kwa
wananchi na kuwahimiza kufanya mazoezi, kupunguza matumizi mabaya ya
pombe na sigara na kuhamasisha upimaji wa afya angalau mara mbili kwa
mwaka,” alisema Profesa Magimba.
Aliongeza kuwa mkakati huo ambao
umesambazwa nchi nzima kupitia kwa Waganga Wakuu wa Mikao yote
unaainisha mikakati tofauti yenye malengo yanayoendana na malengo
endelevu ya maendeleo ya melenia.
“Serikali
imeimarisha tiba katika vituo vyote vya kutolea huduma kwa kuhakikisha
upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na wataalamu, na kuimarisha huduma za
Kibingwa za magonjwa ya moyo katika Taasisi za Bugando, KCMC, JKCI na
ORCI,” Alisisitiza.
Profesa
Magimba aliyataja magonjwa yasiyoambukiza kuwa ni pamoja na Saratani,
magonjwa ya Moyo, magonjwa sugu ya njia ya hewa, Selimundu, magonjwa ya
akili, Figo, Kisukari na baadhi ya magonjwa ya macho.
Akitolea
mfano athari za magojnwa hayo, Profesa Magimba alisema kuwa utafiti
uliofanywa katika ya mwaka 1994 – 2002 ulionyesha kuwa asilimia 18-24 ya
vifo vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza.
Shirika
la Afya Duniani lilikadiria kuwa asilimia 20 ya vifo vyote vilivyotokea
hapa nchini mwaka 2005 vilitokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni tatizo la kimataifa ikijumuisha nchi za Afrika na nchi zinazoendelea. Magonjwa hayo yamesababisha vifo million 36 duniani sawa na asiliamia 63 kwa kipindi cha mwaka 2008.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment