Home » » TFS YAKABIDHI MADAWATI 256 KWA MKUU WA MKOA WA RUKWA

TFS YAKABIDHI MADAWATI 256 KWA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na   Walter    Mguluchuma , Sumbawanga

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),  umemkabidhi Mkuu wa mkoa
wa Rukwa , Zelothe Steven  madawati 256 kwa ajili ya wanafunzi wa
shule  za msingi zilizopo katika  wilaya  tatu  mkoani humo .

Akikabidhi madawati hayo, Meneja wa shamba la Msitu wa Hifadhi  wa
Mbizi , Mohamed Kiangi alisema lengo la wakala huo ni kuunga mkono
juhudi na jitihada za Rais John Magufuli za kumaliza tatizo la uhaba
wa madawati katika shule za msingi na  sekondari.

Kiangi alisema, madawati hayo 256 yaliyokabidhiwa  ni kati ya madawati
 420 yaliyopangwa  kutolewa na TFS kwa mkoa huo  ambapo yatagawiwa
kwa halmashauri za wilaya za Nkasi ,Sumbawanga ,Kalambo na Manispaa ya
Sumbawanga kwa utaratibu  uliowekwa.

Mkuu wa Mkoa huo , Zelothe  mara baada ya kupokea madawati hayo
alisema katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli  mkoa ulifanya
jitihada  kubwa ambapo madawati mapya yalitengenezwa  ingawa bado
kuna upungufu.

Alisema  mkoa  ulikuwa na mahitaji  ya madawati 84,685 ambapo
yaliyotengenezwa  hadi sasa ni madawati 78,072 sawa na asilimia 92.19
ambapo  upungufu ukiwa ni wa madawati  6,613  ikiwa ni sawa na
asilimia 7.8 kwa shule za msingi .

 Aliwataka wakurugenzi  wa halmashauri hizo nne  kuhakikisha
wanasimamia na kuhakikisha madawati hayo yanatunzwa  ipasavyo.

Mwisho.





Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa