WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imezuia majimbo
mawili ya Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini mkoani Rukwa kupewa madawati
1,074 kutokana na kushindwa kuyachukua kwa muda uliopangwa. Aidha,
imewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuwa tayari na safari ya kuhamia
Dodoma ifikapo Novemba 30.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Job Masima,
majimbo 18 yaliyokuwa hayajachukua madawati yao yalipewa siku saba
yafanye hivyo lakini hayo mawili hayakutekeleza agizo hilo lililotolewa
na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Tifa, Dk Hussen Mwinyi.
“Muda wa kuchukua madawati umeisha juzi, napenda kuyapongeza majimbo
16 yaliyoitikia wito na kuchukua jumla ya madawati 8,592. Pia Wizara
imesikitishwa na majimbo mawili yaliyoshindwa kufuata madawati yao,”
alisema.
Madawati hayo ni miongoni mwa yaliyotengenezwa na JKT pamoja na
Magereza nchini baada ya kupewa zabuni na Bunge la Tanzania kutokana na
Sh bilioni sita ambazo chombo hicho kilizirejesha serikalini na Rais
John Magufuli kuagiza zitumike kutengeneza madawati kwa shule nchini.
Kuhusu kuhamia Dodoma, taarifa hiyo iliwataka wafanyakazi waache
kusikiliza maneno ya mitaani badala yake waweke akilini kuwa safari
imeiva na kilichobaki ni utekelezaji.
Katibu Mkuu alisema Serikali imekusudia kuhamishia Makao Makuu yake
mkoani Dodoma, hivyo wizara hiyo inatekeleza maagizo hayo na
inakamilisha taratibu za kuondoka.
“Suala la kuhamia Dodoma halina mahojiano tena kwa sasa, hivyo
mnatakiwa kujipanga ni jinsi gani mtaishi katika mkoa huo kwani
tutaondoka kwa awamu mbili tofauti na awamu ya kwanza itakuwa Novemba 30
na awamu ya pili itakuwa mwezi Juni 2017,” alisema Masima.
Aliongeza kuwa wizara hiyo itahamia Dodoma na baadhi ya Kamandi,
lakini nyingine zitabaki kutokana na umuhimu wa majukumu yake kama
Kamandi ya Wanamaji. Kwa upande wa Makao Makuu ya jeshi hilo, Masima
0 comments:
Post a Comment