Home » » Mbarawa ataka barabara ikamilike ifikapo Julai

Mbarawa ataka barabara ikamilike ifikapo Julai





WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawara ameagiza ujenzi wa barabara ya Sumbawanga –Matai hadi Bandari ndogo ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa, inayojengwa kwa kiwango cha lami, uwe umekamilika ifikapo Julai mwakani.
Amesema hakuna sababu ya ujenzi wa barabara hiyo ya urefu wa kilometa 112 unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 133.2 kuendelea kusuasua wakati fedha zipo.
Alimwagiza mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kukamilisha ujenzi wa mizani, nyumba za watumishi watakaofanya kazi kwenye mizani hiyo na ujenzi wa daraja kufikia Desemba mwaka huu.
Alitoa maagizo hayo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara hiyo unaotekelezwa na mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15, Bereau Group Corporation (CR15G) na Henan Provincial Newcentry Road na Bridge Consultants Limited JV.
Katika hatua nyingine, Mbarawa alisema Serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni 11.6 kwa ajili ya ujenzi wa barabara inayounganisha miji ya Matai na Kasesya wilayani Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2016/17. Alisema mchakato wa kumpata mkandarasi wa kujenga kipande hicho cha barabara chenye urefu wa kilometa 50 unaendelea.
Alisisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kunafungua na kukuza wigo wa biashara kati ya mkoa wa Rukwa na nchi jirani ya Zambia.
“Pia itapunguza kwa kiasi kikubwa mlundikano wa magari makubwa katika Mji mdogo wa Tuduma yanayosafiri kati ya Tanzania na nchi jirani za Kongo DRC na Zambia,” alieleza Profesa Mbawara.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanrods) mkoani Rukwa, Masuka Mkina alisema kazi za usanifu wa kina wa mradi huo zinafanywa na Mhandisi Mshauri , M/s Inter Consult Limited na G –PES Limited kwa gharama ya Sh milioni 400 na usanifu ulianza Januari Mosi, 2014 na kukamilika Januari 31, 2015.
HABARI LEO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa