Home » » TBC KUBORESHA MATANGAZO MIKOA YA PEMBEZONI.

TBC KUBORESHA MATANGAZO MIKOA YA PEMBEZONI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
SERIKALI imesema imeamua kuwekeza kwenye mikoa ya pembezoni kuhakikisha usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) unakuwa mkubwa na wa kutosha kwa maeneo yote nchini.
Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alipofanya ziara jana katika Mkoa wa Rukwa na kukagua mitambo ya kurushia matangazo ya shirika hilo pamoja na kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia.
“Mkoa wa Rukwa ni kati ya mikoa ya pembezoni ambayo usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa ni mdogo hivyo kufanya mikoa hii kusikiliza matangazo ya redio kutoka nchi jirani badala ya kusikiliza taarifa za nchi yetu,” alisema Nape.

Alisema lengo la serikali ni kuwa na vyombo vyenye nguvu ya kusikika mikoa ya pembezoni na ikiwezekana vivuke mipaka na kusikika katika mikoa ya jirani, badala ya wananchi kusikiliza matangazo kutoka vyombo vya nje.
Ili kutimiza lengo hilo, Nape aliahidi kufanya maamuzi magumu kwa kusimamia ubadilishaji wa baadhi ya vifaa, kuhamishia mitambo maeneo ya milimani pamoja na kuweka busta zenye nguvu zitakazoweza kufikisha matangazo ya redio (TBC Taifa) na Televisheni ya taifa (TBC 1) nchi nzima.

Akitoa taarifa kuhusu usikivu wa TBC, mkoa wa Rukwa, Kaimu Mkuu wa Kanda TBC, Nyanda za Juu Kusini, Hosea Cheyo, alisema usikivu wa shirika hilo upo kwa asilimia 75, hivyo kuiomba serikali kuhamisha mtambo wa shirika hilo katika mlima wa King’ombe ili wananchi wa mkoa huo wapate fursa ya kusikiliza redio ya taifa.

Naye Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Lilian Mwangoka aliipongeza Halmashauri ya Nkasi iliyopo katika mkoa wa Rukwa kuwa na redio ya wilaya ijulikanayo kama Nkasi FM inayosaidia kufikisha taarifa kwa jamii.
CHANZO: HABARI LEO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa