Home » » RC ATANGAZA KULALA SAA NNE

RC ATANGAZA KULALA SAA NNE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amesema ili aendane na kasi ya falsafa ya Rais John Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”, atakuwa akilala kwa saa nne kila siku zilizobakia, saa 20 atakuwa kazini akisaka majibu sahihi ya kero zinazowakabili wananchi wa mkoani humo.
Zelothe alibainisha hayo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana kilichojumuisha wazee, viongozi wa dini, watendaji wa umma na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kilichofanyika mjini hapa. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kulala saa nane na kufanya kazi si zaidi ya saa 12 kwa siku.
Alisema aliamua kutumia fursa ya mapumziko ya madhimisho ya Siku ya Karume kuzungumza nao ili kufahamiana na kuelewa vipaumbele vya mkoa huo ambavyo atavisimamia kwa makini, ukaribu na uadilifu.
“Piga ua naahidi nitawasimamia watendaji wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa ili nihakikishe wanaendana na kazi na juhudi za Rais Magufuli kwa kauli mbinu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’. “Msidhani napiga porojo la nitakuwa nalala kwa saa nne tu, muda mwingine uliobakia (saa 20) kwangu ni ‘Hapa Kazi Tu’, isitoshe kazini ninaripoti saa 1:30 asubuhi kila siku za kazi,” alisisitiza Kamishna huyo mstaafu wa Jeshi la Polisi.
Alionya kuwa kwa kila saa atakayokuwa kazini atakuwa na jukumu la kupata majibu sahihi ya maswali sita ambayo ni “nini, wapi, lini, kwa nini, nani na vipi lazima ninapowauliza watendaji maswali hayo nijibiwe tena kwa usahihi mkubwa.” Alisisitiza kuwa lazima watendaji serikalini wamjibu maswali hayo. “Niwahakikishie kuwa katika kupata majibu hayo hakuna jiwe litakaloachwa bila kugeuzwageuzwa ... Lazima libinuliwe kwa kuwa sababu ya kufanya hivyo ipo , uwezo upo pia nia ipo”.
Akisisitiza kuwa maofisa tarafa, kata na vijiji wamegeuka kuwa “miungu watu’ akiwafananisha na ‘kutu ya chuma’ , wameacha kuwatumikia wananchi badala yake wamegeuza kazi zao kuwa mitaji yao ya kujitajirisha wakiwakera na kuwakatisha tamaa wananchi.
Awali akimkaribisha Msaidizi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa (Tamisemi), Albinus Mgonya alieleza kuwa RC ameonesha njia na dira ya kufuata katika utendaji wa kila siku wa watumishi wa umma. Wazee walieleza kuwa watampatia ushirikiano wa kutosha ili asimamie vyema nidhamu na uwajibikaji serikalini.
CHANZO: HABARI LEO.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa