Home » » TAASISI YA BENJAMINI WILIAMU MKAPA YAKABIDHI NYUMBA 20 KWA MIKOA YA KATAVI NA RUKWA

TAASISI YA BENJAMINI WILIAMU MKAPA YAKABIDHI NYUMBA 20 KWA MIKOA YA KATAVI NA RUKWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi
Taasisi ya  Benjamini Wiliam Mkapa  imekabidhi  nyumba 19  kwa Halmashauri za Mikoa ya Katavi na Rukwa  kwa ajiri ya watumishi wa Idara ya afya  zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi  Biloni 1.3.
Makabidhiano ya nyumba hizo yalifanyika juzi katika zahanati ya Kabungu Wilayani Mpanda kwaniaba ya nyumba nyingine zilizojengwa katika Halmashauri za mikoa ya Katavi na Rukwa ambapo mgeni Rasmi  alikuwa  Waziri Mkuu msitaafu  wa awamu ya nne Mizengo Pinda.
Katika Risara iliyosomwa  na  Asifa Mtendaji mkuu wa Taasisi  ya Benjamini Wiliam Mkapa Dkt  Ellen  Senkoro  alisema wakati taasisi hiyo inaadhimisha miaka kumi  ya kazi zao  wamechangia  jitihada mbalimbali za Serikali hapa nchini  ikiwemo mikoa ya Rukwa na Katavi.
 Alisema  mbali ya ujenzi wa nyumba hizo za watumishi wa afya pia  Taasisi hiyo  imeajiri watumishi 63  na kuwapeleka katika mikoa hiyo miwili ambao wamekuwa wakitowa huduma  za tiba na maabara  katika Hospitali na  vituo  vya afya vya Serikali .
Pia  wameimarisha  vyuo vya mafunzo  vya afya  kwa kuajiri  na kupeleka  walimu 8 katika vyuo  vilivyopo katika Mkoa wa Rukwa  kwa nia ya kuhakikisha  vyuo hivyo  vinapata  uwezo mkubwa  zaidi  wa  kudaili na kufundisha wanafunzi wa  kada za afya nia kuongeza  uzalishaji  zaidi   ya wataalamu wa afya nchini.
Dkt  Senkoro alisema  kuhusiana na mradi huo wa ujenzi wa nyumba  Serikali  ya Tanzania  kupitia Wizara  ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia  Wazee na Watoto  waliamua  kuendelea  kushirikiana  na Taasisi ya  Mkapa  katika kutekeleza  mradi kuanzia mwaka 2011 hadi 2016 mradi huo unalenga kuimarisha  mfumo wa  sekta ya afya .
Alisema Taasisi hiyo mpaka sasa imejenga  nyumba  480 hapa nchini kati ya nyumba hizo nyumba 40 zipo katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
Waziri Mkuu msitaafu Mizengo Pinda  alitowa shukurani kwa Taasisi ya Mkapa  kwa kuratibu na kupatikana kwa msaada  huo  mkubwa .
Pinda  alisema  Serikali yetu  licha ya mafanikio  yaliyopatikana  nchi yetu  bado inakabiliwa  na tatizo kubwa  la upungufu wa watumishi wa afya  hasa vijijini  nale  yasiyofikika kwa urahisi .
Pia aliwataka watumishi wanaopangiwa kazi katika  mikoa ya Katavi na Rukwa kuacha imani potofu  kuwa mikoa hiyo inauchawi hari ambayo imepelekea watumishi wanaopangiwa kazi kushindwa kulipoti.
Muuguzi wa Zahanati ya Kabungu Rose Mpimbe alisema    nyumba waliyokadhiwa itawafanya wananchi wa Kata ya Kabungu kupata huduma kwa muda wote kwani walikuwa wakishindwa kutowa huduma kwa wagonjwa kutokana  zahanati hiyo kutokuwa na nyumba ya kuishi mganga wala wauguzi ambao wote walikuwa wamepanga nyumba kijiji cha jirani cha Kagwila kilichopo umbali wa kilimeta mbili

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa