Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jaji Mfawidhi
wa Mahakama ya Tanzania kanda ya Sumbawanga
Jaji Kakusulo Sambo amewapongeza Mahakimu wa Mahakama za
mwanzo wa Kanda ya Sumbawanga kwa kufikia
lengo la kutokuwa na shauri hata moja lenye umri wa zaidi ya mwaka
mmoja ambalo halijasikizwa
Pongezi hizo alizitowa
hapo jana wakati alipokuwa akifungua
kikao cha baraza
la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania
Kanda ya Sumbawanga kilichofanyika
katika ukumbi wa idara ya maji Mjini Mpanda Mkoani Katavi
Alisema takwimu
za Mahakama za mwanzo zinaonyesha kuwa kwa kanda
nzima ya Sumbawanga kwa
mwaka wa 2014 mashauri
yote 5177 yalifunguliwa katika Mahakama hizo
ziliweza kusikilizwa
mashauri hayo
yaliokuwa yamefunguliwa yalipunguza
deni ambazozilikuwa hazijasikilizwa mwaka 2013 kwa asilimia 2.0 sawa na
mashauri 105 kati ya mashauri 1042 yaliyokuwa yamebaki mwaka 2013
Alifafanua kuwa Mahakama imeisha weka mwongozo wa kila jaji
na Hakimu kumaliza idadi fulani
ya mashauri anayopaswa kuyasikiliza
na kuyatolea maamuzi kwa mwaka mzima
Jaji Sambo
alisema kila Jaji ameishapangiwa
kusikiliza na kumaliza
mashauri 220 Hakimu wa Wilaya na
Mkoa mashauri 250 na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo
mashauri 260 kwa mwaka mzima
Alisema ili
Mahakimu waweze kumaliza kesi
za watu kwa wakati ni
lazima wawajibike na
waongeze kiwango cha uwajibikaji wa kazi
yao hiyo ya uhakimu
Jaji Sambo
alieleza kuwa kitendo cha
Mahakama kumcheleweshea
mtu kesi ni
chanzo cha kumkwamishia mtu maendeleo yake na
imekuwa ikiathili jamii
Nae Naibu
msajiri wa wa Mahakama kuu Sumbawanga Romali
Mbuya alieleza kuwa jumla ya
mashauri 228 yalifunguliwa
katika kipindi cha mwaka 2014
katika mahakama kuu kanda ya Sumbawanga
ambapo kesi za jinai zilikuwa 134 madai
94 na ambazo zimeishwa zikilizwa mpaka sasa ni 224 sawa na asilimia 98.2
Alisema takwimu za
mahakama za Wilaya zinaonyesha
kuwa kanda ya Sumbawanga haina mzigo
wa mashauri mengi yanayopokelewa kwa mwaka
Alifafanua kuwa
ni Wilaya ya Mpanda pekee ndio
zipo kesi nyingi zilizopokelewa kwa mwaka ukilinganisha na Wilaya nyingine za
kanda ya Sumbawanga hata hivyo
Mahakimu hao wameweza kumaliza kwa
kiasi kikubwa kesi hizo
Alieleza kwa mwaka 2014
yalifunguliwa mashauri 1545
katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda
yenye Mahakimu watatu na kesi
zilizosikilizwa zilikuwa ni
1,601 kesi ambazo zilikuwa zimebaki mwaka 2013 zilikuwa ni 326 kesi hizo zilisikilizwa na kuamuliwa na
hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo
Chiganga Ntengwa ambae kwa kipindi
kirefu cha mwaka jana alikuwa peke yake kesi
zilizobaki hadi sasa ambazo
ni za miaka ya nyuma ni 270
Alifafanua
Sumbawanga walikuwa na
jumla ya mashauri
546 kwa mwaka kwa idadi ya mahakimu
saba walipo katika
Mahakama ya Sumbawanga ni wazi kuwa kila Hakimu alikuwa
na wastani wa mashauri
78 kwa mwaka
Alisema kila
hakimu alikuwa alikuwa na
mashauri 46 tuu kwa mwaka mzima
kiwango hicho ni cha chini sana ya kiwango
cha kitaifa ambacho ni mashauri 250 hii inamaana kuwa
Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga
haikupaswa kubaki na shauri hata moja
endapo kila hakimu
angesikiliza mashauri 78
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment