Na Walter Mguluchuma.
Rukwa yetu
WATU
watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Rukwa,likiwemo la
mwanamke mmoja kumuua memewe kwa kupiga kichwani na mtwangio wa kinu.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda tukio hilo
lilitokea feb 4 mwaka huu nyakati za saa asubuhi ya alfajiri baada ya
kuzuka kwa ugomvi wa kifamilia baina yao.
Alisema kuwa
inasemekana kwamba mwanamke huyo aitwaye Clemencia Nowa (50) kwa muda
mrefu alikuwa ana maelewano na mumewe Stephen Shauri (72) hivyo asubuhi
hiyo kulitokea mzozo baina yao uliosababisha kutokea kwa ugomvi mkubwa.
Ugomvi
huo ulimfanya mwanamke kukimbilia mtwangio wa kinu (mchi) kisha kumpiga
nao kichwani mwenza wake hali iliyosababishia kuanguka na kufariki
dunia papo hapo.
Katika tukio jingine, mkazi wa kijiji
cha kipande tarafa ya kate, wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, amefariki
dunia baada ya kupigwa na radi akiwa amejificha chini ya shambani wakati
mvua kubwa ikiendelea kunyesha.
Inadaiwa kuwa wakati mvua hiyo
ikinyesha mwanamke huyo aitwaye Hellena Kauzeni (36) alikuwa akiendelea
na shughuli zake za kilimo shambani kwake lakini ilipozidi alikwenda
kujificha chini ya mti ndio radi zilizokuwa zimeambatana na mvua hiyo
zipompiga na kumsababishia kifo chake.
Wakati huo huo,
kijana mmoja mkazi wa katandala alifahamika kwa jina moja la utani
Nokia amekutwa amefariki dunia akiwa amelala chumbani kwake, ambapo
mwili huo uligundulika feb 5.
Kamanda Mwaruanda
alisema kuwa kwa tukio la mwanamke kumuua mmewe tayari mwanamke huyo
amekamatwa na anahojiwa tayari kwa kufikishwa mahakamani ili kujibu
tuhuma zinazomkabili ila kwa matukio mengine uchunguzi bado unaendelea.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment