Home » » WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Rukwa

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Rukwa


WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Rukwa, likiwemo la mtoto mmoja kupigwa na radi wakati akifanya shughuli za uvuvi na baba yake mzazi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda tukio la kijana huyo kupigwa na radi hadi kufariki lilitokea juzi nyakati za saa moja asubuhi katika kijiji cha Kasanga mwambao wa ziwa Tanganyika  na kumtaja mtoto huyo kuwa ni Owden Sikazwe (15).
Alisema kuwa kijana huyo akiwa na baba yake mzazi  aitwaye Sikazwe Owden na mtu mwingine aliyefahamika kuwa ni Aman Ntayanga ambapo walikuwa katika mtumbwi wakielekea kutegua nyavu walizoweka kwa ajili ya kunasa samaki ndipo radi hiyo hiyo ilipowatupa pembeni watu hao na kupiga kijana huyo na kumzamisha hivyo  kumsababishia kifo papo hapo.
Kamanda Mwaruanda alisema kuwa katika tukio jingine, mwanafunzi wa mwaka wa pili, chuo cha ualimu Rukwa Zakayo Anyosisye (25) amekutwa amefariki dunia katika kumbi ya kuonyesha mpira kwake huko maeneo ya Chanji B mjini hapa.
Taarifa zinaeleza kuwa siku ya tukio nyakati za usiku baada ya watu kutazama mpira alifunga ukumbi huo uliokuwa akiusimamia na yeye kuingia kulala ukumbini humo.
Inasemekana kwamba  ilipofika nyakati za asubuhi, majirani walikuta mlango wa ukumbi umevunjwa na huyo mwanafunzi akiwa humo ukumbini tayari amefariki huku akiwa na jeraha la kupigwa na kitu kizito kichwani
Kamanda wa Polisi Mwaruanda  alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika hadi sasa ila polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, ili waliohusika waweze kusakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili ichukuwe mkondo wake.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa