Home » » SERIKALI inafanya mchakato wa uanzishwaji wa wilaya ya kipolisi

SERIKALI inafanya mchakato wa uanzishwaji wa wilaya ya kipolisi


Na  Walter  Mguluchuma
Rukwa yetu Blog
SERIKALI inafanya mchakato wa uanzishwaji wa wilaya ya kipolisi itayohudumia wananchi wa mji mdogo wa laela mkoani Rukwa na vijiji vinavyopitiwa na barababara ya Tunduma hadi Sumbawanga na maeneo mengine ili kusaidia kudhibiti uhalifu wa kutumia silaha ulioshamiri katika maeneo hayo.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema hayo jana wakati hafla fupi ya akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha polisi cha kisasa cha Laela kilichojengwa kwa msaada wa Taasisi mfuko wa changamoto za milenia hapa nchini (MCA-T) kwenye mji wa Laela wilayani Sumbawanga.

Manyanya alisema kuwa imeonekana ipo haja ya uanzishwaji wa wilaya mpya ya kipolisi katika mkoa wa Rukwa ambao upo mpakani na jirani ili kusaidia kudhibiti ongezeko la matukio ya ujambazi ambao umekuwa ukihatarisha maisha ya watu pamoja na mali zao.

Alisisitiza kuwa licha mkoa huo kuwa mpakani ambako mara nyingi kumekuwa kukifanyika matukio ya uhalifu kutoka upande wa nchi moja na wahalifu kukimbilia nchi nyingine bado upo ulazima wa kuimarisha ulinzi hasa baada ya kukamilkja kwa ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga inayowapa urahisi pia wahalifu kufanya ujambazi eneo moja na kwenda kujificha jingine.

"Kupitia mpango wa Rukwa salama ulioanzishwa 2012 nimekuwa na ndoto ya kutokomeza mateso ya uhalifu na unyanyasaji wa aina yoyote ikiwemo imani za kishirikina sasa basi kuanzishwa kwa wilaya ya kipolisi kutakuwa chachu ya kupambana kikamilifu na uhalifu huo na kuifanya Rukwa kuwa eneo salama hivyo wananchi wake kuishi kwa amani na utulivu muda wote" alisema Manyanya.

Awali, Naibu afisa wa mtendaji wa mkuu wa MCA-T, Paschal Assey alisema kuwa lengo la kujenga vituo hivyo vya polisi vilivyogharimu zaidi ya Sh milioni 379 ni kuimarisha usalama wa raia pamoja na mali zao katika maeneo yanayopitiwa na barabara ya Tunduma - Sumbawanga ambayo unatembea umbali mrefu bila kuwepo kwa kituo chochote cha polisi kitu ambacho si sahihi.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa ujenzi wa vituo hivyo viwili vya polisi ni chachu ya kutaongeza ari ya utendaji wa polisi hivyo kuwafanya afanye kazi zao ufanisi mkubwa wenye kuleta tija kwa jamii wanayoihudumia.

Mwaruanda aliongeza kuwa pamoja na kuwa na vituo hivyo vya kisasa lakini bado ushirikiano baina polisi na wananchi unahitajika hasa katika kutoa taarifa za siri kuhusu uhalifu kwani ndio utasaidia kudhibiti hali hiyo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa