Home » » Hospitali Rukwa yakabiliwa na changamoto lukuki.‏

Hospitali Rukwa yakabiliwa na changamoto lukuki.‏


Walter Mguluchuma .
Sumbawanga.

HOSPITALI teule ya Dr Atman ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wodi za kulaza wagonjwa kiasi cha kusababisha watoto wachanga kulazwa pamoja na watu wazima kitu ambacho ni hatari zaidi kiafya kwa watoto hao.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Aaron Hyera alisema hayo jana wakati akitoa taarifa fupi ya hospitali hiyo kwa Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa, Symthies Pangisa wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitanda 10 na mashuka 50 kutoka mfuko wa Penisheni kwa watumishi Umma (PSPF) vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni tano zilizofanyika katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa hospitali hiyo ambayo ipo chini ya kanisa katoliki jimbo la Sumbawanga, inakabiliwa na changamoto hiyo hivyo baadhi ya wagonjwa ambao ni watoto wachanga na watu wazima ulazimika kulala pamoja hali ambayo ni hatari zaidi kwa watoto hao kwani kutokana na kuwa na kinga ndogo wanakuwa katika hatari kubwa ya kupata maradhi mengine kutoka kwa wagonjwa wengine.

Dk Hyera alisema kuwa katika kukabiliana na  changamoto hiyo tayari uongozi wa hospitali hiyo unaendelea na ujenzi jengo la wodi ya watoto kwa fedha za mkopo kutoka Shirika la bima ya afya (NHIF) ambao waliwakopesha sh milioni 120.
Alisema licha ya kupata mkopo huo lakini bado fedha hizo hazitoshelezi kufanikisha ukamilishaji wa kazi hiyo, hivyo wanaendelea kuomba msaada kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo watu binafsi wenye moyo wa kusaidia wajitokeze kuwasaidia baadhi ya vifaa vya kukamilisha ujenzi, vifaa tiba na madawa kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Awali, Akikabidhi msaada huo, afisa Mfawidhi wa mfuko wa Penisheni kwa watumishi wa umma (PSPF) mkoa wa Rukwa, Paul Mbijima alisema kuwa kwa kuwa mfuko wa Pspf umetoa msaada huo ukiwa sehemu ya kurudisha kile wanachokipata kutokana kwa jamii lakini kuonyesha kwamba unathamini na kujali afya ya wachangiaji wake.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Pangisa licha ya kuishukuru Pspf kwa msaada huo pia alisema kuwa umefika wakati sasa mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachopitapa kwa jamii.
 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

1 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa