Home » » HATMA YA WANAOTUHUMIWA KWA RUSHWA CCM YANUKA

HATMA YA WANAOTUHUMIWA KWA RUSHWA CCM YANUKA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
 
Hatma ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaodaiwa kumwaga fedha kwa wajumbe wa wa vikao vya chama hicho huenda ikajulikana mwishoni mwa wiki hii.
Makada hao wanadaiwa kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Vikao vya chama hicho vinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Taarifa za vigogo kugawa fedha kwa wajumbe hao zimekuwa zikitolewa na hivi karibuni, mitandao kadhaa ya kijamii iliripoti kuwa kigogo mmoja wa chama hicho alikuwa akigawa fedha kwa makada huko Zanzibar.

Kufuatia taaifa hizo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, aliagiza Tume ya Maadili ya chama hicho kuchunguza ugawaji wa fedha hizo ambazo, kila Mjumbe wa NEC alipatiwa Sh. milioni moja na Sh. 500,000 kwa kila Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, aliliambia NIPASHE kuwa, Kamati Kuu ya CCM inatarajia kukaa vikao vyake mwishoni mwa wiki.
“Hatima ya suala hilo unaweza kuifahamu baada ya vikao vitakavyoanza Jumamosi (kesho), kama suala hilo linaweza kuwa ajenda ya kujadiliwa ndani ya vikao vyetu,” alisema Nchemba.

Hata hivyo, alisema yeye siyo msemaji wa chama, hivyo taarifa kamili zinaweza kupatikana kutoka kwa msemaji wa chama mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Jumamosi jioni.

Hata hivyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipolizwa jana kuhusu hatima ya vigogo wanaotuhumiwa kugawa fedha zikiwamo tuhuma za aliyeyagawa zedha Zanzibar, alisema taarifa kamili zinaweza kupatikana mara baada ya vikao vya chama kumalizika.

Alisema kuwa: “Nafikiri tusubiri vikao vya chama vimalizike ndipo nitatoa taarifa kwa sababu hili suala sina taarifa nalo vizuri. Pia bado sijafahamu ajenda za vikao vinavyotarajia kuanza hivi karibuni kwa hiyo sijui kama tutalijadili.”

Alifafanua kuwa, suala la vikao kuwa vitaanza lini atalizungumza leo.

Vikao vya hivyo vinaanza wakati ambao makada wake sita waliofungiwa na Kamati Kuu chama hicho(CC) wanakaribia kifungo chao cha mwaka mmoja.

Februari mwaka jana, CC, ilitangaza kuwafungia kwa miezi 12 wanachama wake sita baada ya kubainika kuanza kufanya kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati.

Wanachama waliofungiwa kutojishughulisha na masuala ya chama na kuwekwa chini ya uangalizi mawaziri wakuu wastaafu, Mkuu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Makada hao pia walipewa adhabu ya kutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama kwa miezi 12.

Kadhalika makada hao walipewa na onyo kali kwa mujibu wa Ibara ya 6(2) (1-5) ya Maadili ya Viongozi wa CCM ambayo inawazuia kutoa michango, misaada, zawadi ya aina yeyote, kukusanya michango na kufanya kampeni yeyote bila ya kupata kibali kutoka kwa kamati kuu ya siasa ya halmashauri ya eneo husika.

Aidha chama kiliagiza kuwa wanachama hao wanaweza kujikosesha sifa za kugombea nafasi yoyote ndani ya chama kama watakiuka maagizo hayo CC.
 
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa