Home » » Taasisi moja isiyo ya kiserikali mkoani Rukwa CEELS linalojishughulisha na uboreshaji wa huduma za kiuchumi za kijamii na msaada wa kisheria limetoa ushauri kwa viongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoani Rukwa kuimarisha utoaji wa elimu sahihi ya uzazi wa mpango

Taasisi moja isiyo ya kiserikali mkoani Rukwa CEELS linalojishughulisha na uboreshaji wa huduma za kiuchumi za kijamii na msaada wa kisheria limetoa ushauri kwa viongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoani Rukwa kuimarisha utoaji wa elimu sahihi ya uzazi wa mpango


Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga

Taasisi  moja siyo   ya  kiserikali mkoani Rukwa CEELS linalojishughulisha na uboreshaji wa huduma za kiuchumi za kijamii na msaada wa kisheria limetoa ushauri kwa viongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoani Rukwa kuimarisha utoaji wa elimu sahihi ya uzazi wa mpango ili uwezo wa  kiuchumi wa kila kaya ulingane na ukubwa wa idadi ya watu katika familia moja

Mratibu  wa kitengo cha utafiti cha Taasisi hiyo Willian Nathan alitoa kauli hiyo wakati wakilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya hivi karibuni kwenye kiijiji cha Kisumba ya watoto kilichopo kata ya Kisumba ili kutekeleza kauli mbiu isemayo boresha uzalishaji na usalama wa chakula kwa lishe bora

ALISEMA utafiti uliozihusisha kaya za wananchi wanaoishi katika vijiji 9  vinavyounda kata ya Kisumba umegundua kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula na pia njia mbalimbali za kujipatia kipato cha kila kaya hakilingani na idadi ya watu wanaounda familia moja hali aliyosema inazorotesha afya za wanafamilia na kuishi katika hali ya umaskini

 Nathan alisema CEELS iliamua kuwa na wiki ya maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika kwenye kijiji cha Kisumba kutokana na utafiti unaodhihirisha kuwapo kwa kasi kubwa ya uzazi katika kijiji hicho na vingine 8 vinavyounda kata hiyo ikilinganishwa na maeneo mengine ya vijiji  vya wilaya hiyo ya Kalambo

Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya afya inatakiwa kuwa na mpango mkakati endelevu wa kuhakikisha kila familia inakuwa na mpango wake madhubuti wa kuwa na idadi stahili ya watoto kwa kuzingatia uwezo wake wa kiuchumi badala ya kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaokuwa mzigo katika malezi na kukosa huduma muhimu za kijamii ambazo ni pamoja na elimu mavazi na huduma nyingine za afya

Mmoja wa waelimisharika wa CEELS aliyeshiriki kutoa mafunzo ya jinsi ya jinsi ya kuboresha uzalishaji wa vyakula Happyness Dawson alisema baadhi ya wanachi katika vijiji hivyo vya kata ya Kisumba wanashindwa kuwa na mpango mzuri wa lishe bora kutokana na kiasi kidogo cha mazao ya chakula inayozalishwa  ikilinganishwa na idadi kubwa ya watu katika familia moja

Alisema kutokana na hali hiyo ya watoto wengi wenye umri wa chini ya miaka mitano hupata magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na  utapiamlo napia kusababisha afya ya mama na baba kutokuwa imara kwa kukosa lishe bora kutokana na uzazi wa karibu kila mwaka unaowafanya washindwe kupanga mipango sahihi ya huduma za afya na pia elimu kwa watoto wao

Afisa mtendaji wa kata hiyo Nelly Gervas alisema katika taarifa yake katika kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika kuwa vijiji 9 vya kata ya Kisumba vya Kapozwa Mpombwe Ngorotwa Nondo Kisumba Kasote Chisenga Kafukoka na Kachele vina jumla ya watoto chini ya umri wa miaka mitano zaidi ya 98 elfu ikilinganishwa na idadi ya watu wazima kiasi cha elfu 23

Alieleza  ndio maana hata jina la kijiji cha Kisumba limebadilika na kuitwa na watu mbalimbali kuwa Kisumba ya watoto kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa bila kuzingatia uwezo sahihi wa kila kaya ambapo alisema kwa wastani familia yenye kuwa na idadi ndogo ya watoto huwa ni watoto watano
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa