Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga
Serikali imeanzisha utaratibu wa kuvitumia
vikundi vya wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kuvikopesha pembejeo za
ruzuku kuanzia msimu ujao wa kilimo 2014/2015 kwa ajili ya wakulima katika
maeneo yao ili kukabiliana na vitendo
vya udanganyifu vilivyokuwa vinafanywa na
baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu katika misimu ya kilimo
iliyopita
Afisa pembejeo wa wilaya ya Kalambo mkoani
Rukwa Gothard Lyampawe aliwaambia wakulima na wanachama wa chama cha ushirika
cha msingi cha mazao na masoko kitwacho Muzia AMCOS cha mji mdogo wa Msanzi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wakati wa kikao
cha mkutano mkuu wa chama hicho kuwa utaratibu huo utamwezesha kila mkulima
kupata ruzuku stahili kwa wakati bila usumbufu
Lyampawe aliwaambia wanachama hao na
pia baadhi ya wakulima waalikwa kutoka vyama vya ushirika sita vya kata za Sopa
Mkali na Matai za wilaya ya Kalambo ikiwa ni pamoja na maafisa ugani wa kata
hizo na wadau wa kilimo na mashirika
yanayosambaza mbegu na mbolea mkoani Rukwa kuwa serikali itasimamia kikamilifu utaratibu
huu ili kumwezesha mkulima kulima kilimo endelevu cha faida na biashara
Alifafanua baadhi ya wakulima wanadaiwa
kukatishwa tamaa na jinsi serikali ilivyoshindwa kuthibiti ujanja wa baadhi ya
wasambazaji wa ruzuku za kilimo na hivyo kulazimika kuendesha shughuli zao za
kilimo kwa gharama kubwa kuliko faida wanayoipata mara baada ya mavuno yao
Nae afisa kilimo wa wilaya ya Kalambo Nicholas
Mrango ambaye katika mkutano huo alimwakilisha mrajisi wa vyama vya ushirika
mkoa wa Rukwa alisema vyama vya ushirika vitakuwa na dhamana kwa wanachama wao
kwa kuhakikisha pembejeo za ruzuku zinawafikia wakulima bila usumbufu kwa
kuingia mikataba yenye tija kwao badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara hao
Alisema umeandaliwa
utaratibu utakaozishirikisha bodi za vyama vya msingi vya ushirika katika
kuanisha makampuni yenye sifa kwa ajili ya kuwasambazia pembejeo za kilimo kwa
bei nafuu na kwa wakati ili kumnufaisha mkulima
Wakati wa kufungua mkutano huo mwenyekiti
wa Muzia AMCOS Linus Patrick alisema mkutano huo mkuu umewashirikisha wakulima
na wadau mbalimabli wa kilimo ikiwa ni wasambazaji wa mbolea mbegu na madawa ili kushiriki kwa pamoja
kutatua changamoto zinazoukabili
ushirika katika kuboresha ustawi wa wanachama
Mmoja wa wadu wa kilimo mashirika
yanayosambaza pembejeo mbalimbali za kilimo mkoani Rukwa na Katavi Michael Rukanga wa kampuni ya mbegu ya
SEEDCO na Magnus Chaula wa kampuni ya
mbolea aina ya YARA walisema wataanzisha mashamba darasa katika maeneo
mbalimbali wilayani Kalambo ili kutoa elimu stahili na sahihi kwa wakulima
jinsi ya kutumia mbegumbolea na madawa kwa faida ya kuongeza uzalishaji wa
mazao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment