Home » » PINDA:NIMETANGAZA URAIS KIMYAKIMYA

PINDA:NIMETANGAZA URAIS KIMYAKIMYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza rasmi kugombea urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa mwakani huku akisema amejitangaza kimyakimya.

Pinda aliliambia Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza juzi usiku kuwa atakuwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho watakao wania nafasi hiyo.

Pinda ambaye yupo mjini London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa viongozi unazungumzia uwekezaji zaidi katika bara la Afrika.

“Wamejitokeza wengi, lakini na mimi nimo japo ile kimya kimya imekuwa ikiendelea,” alisema Pinda akimaanisha kuwa harakati za siri siri zimekuwa zikiendelea kufanikisha mikakati yake hiyo.

Pinda alisema pamoja na kwamba wamejitokeza watu wengi kutaka kuwania nafasi hiyo, lakini inaweza ikashika na mtu yeyote ambaye mwisho wa safariataonekana ana sifa kulingana na taratibu za ndani ya chama na serikali.

Alisema waliojitokeza watachunjwa katika mikutano ndani ya chama na hatimaye wananchi watapiga kura Oktoba mwakani na wagombea wa vyama vingine kuchagua mmoja ambaye ndiye atakuwa rais.

Makada wengine waliojitokeza hadharani kutangaza kuwania nafasi hiyo ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Nzega,Dk. Hamis Kingwangalla.

Kwa mara ya kwanza, Pinda aliripotiwa kutangaza nia yake jijini Mwanza alipowaalika wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM  kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, ingawa tangu wakati huo hakuwahi kuthibitisha wala kukanusha.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa