Home » » KAMANDA WA UVCCM WILAYA YA KALAMBO ANENA

KAMANDA WA UVCCM WILAYA YA KALAMBO ANENA

Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga

Kamanda  wa vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi –UVCCM- wilaya ya Kalambo Rosweeter Kasikila ameelezea jinsi viongozi walioteuliwa hivi karibuni kuwa makamanda wa vijana katika ngazi za kata wanavyotakiwa kuwa wabunifu kwa  kuandaa mazingira mazuri ya kiuchumi yatakayowezesha kuundwa kwa vikundi vya vijana vya wajasiliamali ikiwa ni moja ya mbinu za kukabiliana na umaskini na kujiepusha na vitendo vya uhalifu

Akizungumza na vijana wa CCM wa kata ya Matai kwenye mji mdogo wa Matai makao makuu ya wilaya ya Kalambo baada ya kukamilika zoezi la kuwasimika makamanda wa kata 17zinazounda tarafa 5 za wilaya hiyo alisema makamanda hao wa kata wana wajibu wa kuwahudumia vijana katika kata zao bila kujali itikadi zao za  vyama vya siasa na kuwahamasisha juu ya elimu ya kujitegemea

Alisema  uamuzi huo wa kuwateua makamanda hao katika ngazi za kata unalenga kukabiliana na wimbi la vijana wengi wanaomaliza elimu katika shule za msingi na sekondari kukosa fursa ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu na kujikuta wanajihusisha katika vitendo mbalimbali vya uhalifu

 Kasikila ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi mkoani Rukwa alisema changamoto inayowakabili vijana hivi sasa ni jinsi ya kupata mitaji ya kuanzisha miradi ya kiuchumi kutokana na kukosa umoja utakaowawezesha kuaminika na vyombo mbalimbali vya fedha na hata halmashauri za wilaya ambazina  utaratibu wa kuvisaidia vikundi vya vijana na wanawake

Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kalambo Cledo Mpondela aliyekuwa kiongozi  wa kuwasimika makamanda hao wa kata alisema alipewa jukumu hilo la kuwapa mamlaka hayo ya kichama ili  kujenga fikra za kuajiriwa miongoni mwa vijana na kuwawezesha kujipanga kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ambavyo itakuwa rahisi kwao kukopesheka

Allsema makamanda hao waliosimikwa kupitia jumuia ya vijana wa CCM watakuwa na jukumu la kusimamia mipango yote ya maendeleo ya vijana kiuchumi na pia kushiriki katika hamasa za masuala ya kitaifa yanayolenga kuwapiga vita maadui ujinga maradhi na umaskini licha vilevile kujihusisha na utekelezaji wa sera za Chama Cha Mapinduzi

 Mpondela alisema utaratibu huu wa kuwasimika makamanda wa vijana katika kata zote za wilaya hiyo ya Kalambo ni maagizo yanayotekelezwa katika wilaya zote za mkoa wa Rukwa na Taifa kwa ujumla kwa lengo la kusaidia kuwaunganisha vijana katika masuala yao ya kiuchumi na pia kisiasa

Aliwataka vijana wote wilayani Kalambo na wananchi kwa ujumla kuanza kujipanga kuzitumia fursa za kimaendeleo zilizopo hivi sasa wilayani humo ambazo ni kuanzishwa kwa wilaya mpya na ujenzi wa barabara za lami kutoka makao makuu ya Mkoa mjini Sumbawanga kwenda bandari ndogo ya Kasanga inayounganisha wafanyaniashara wa nchi za Tanzania na zile za maziwa makuu za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Burundi na Rwanda

 pia aliitaja barabara nyingine kuwa ni ile iendayo mji wa mpakani na nchi ya Zambia wa Kasesya na pia mradi kabambe wa usambazaji wa umeme vijijini REA ambao utavinufaisha vijiji vingi vya wilaya hiyo na hivyo kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji mali kupitia vikundi vya ushirika ya kiuchumi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa