Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Rukwa,
imekitaka chama hicho kuwa makini katika kutathimini uwezo na
kukubalika kwao katika jamii wagombea wa nafasi mbalimbali katika
chaguzi zijazo za Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Rukwa, Rainer Lukara, alisema
hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha jumuiya hiyo kilichofanyika
juzi mjini hapa.
Alisema kuwa, iwapo CCM itakuwa makini katika kuwatathimini wagombea
wake watakaojitokeza kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ni wazi
haitakuwa kazi ngumu kuwanadi mbele ya jamii.
"Hatutaki kupata shida tena kama ilivyokuwa chaguzi zilizopita,
kwani baadhi ya wagombea walipata upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa
vyama upinzani…..ni wakati sasa chama kuangalia sifa, uwezo, uadilifu
na namna wagombea wanavyokubalika kwenye jamii," alisema Lukara.
Awali, mgeni rasmi katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi Mkoa wa Mbeya, Fatuma Katila, alionya kuhusu makundi na
migawanyiko isiyo na tija na tamaa za wachache katika kutaka uongozi
kwa maslahi binafsi badala ya umma.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment