Walter Mguluchuma
Sumbawanga.
UJENZI wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na
Shirika la nyumba la taifa (NHC) umetajwa kwanba ni chachu kwa
halmashauri za wilaya mkoani Rukwa kutoa maeneo ya kutosha ili shirika
hilo liweze kujenga nyumba ambazo zitashawishi watumishi wengi kukubali
kuishi katika maeneo mengi ya mkoa huo unaokimbiwa na watumishi kwa
kisingizio cha mazingira magumu ya utendaji wa kazi.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka alisema hayo ambaye
alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya wakati kwenye
makabidhiano ya mashine 16 za kufyatulia matofali kwa vijana zaidi ya
200 wa halmashauri zote nne za mkoa huo zilizotolewa na Shirika la
nyumba la taifa katika hafla fupi iliyofanyika mjini hapa.
Sedoyeka alisema kuwa mara kadhaa watumishi wanaopangiwa kwenda
Rukwa ukataa kurejea kazini mara baada ya kuripoti kwa kisingizio cha
mazingira magumu ya utendaji wa kazi na ukosefu wa nyumba za kuishi
hivyo sasa mpango wa ujenzi huo wa nyumba za NHC uwe chachu kwa
halmashauri hizo kuchangamkia fursa hiyo kwa kutoa maeneo ya kutosha ya
ujenzi wa nyumba hizo.
"Nachokiamini ni kwamba ujenzi wa nyumba hizi ukikamilika watumishi
wengi watashawishika kukaa Rukwa, kisingizio cha mazingira magumu ya
kazi, ukosefu wa nyumba hazitakuwepo ukizingatia kwamba pia kuna ujenzi
wa barabara ya Sumbawanga hadi Tunduma kwa kiwango cha lami umekamilika"
alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Awali, Meneja wa shirika la nyumba la taifa mikoa ya Rukwa na Katavi,
Nehemia Msigwa alisema kwa NHC inatekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba
bora za makazi na biashara itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 8.7
kwenye manispaa ya Sumbawanga, Mpanda, Mlele na Nsimbo kwa lengo la
kukabiliana na tatizo
kubwa la makazi hasa kwa watumishi.
Msigwa alisema kuwa ili
kufanikisha mpango huo, shirika kwa kushirikiana na wakala wa utafiti wa
vifaa bora vya ujenzi wa nyumba (NHBRA) iliyo chini ya wizara ya ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi, pamoja na mamlaka ya elimu na ufundi
stadi (VETA) ilitoa mafunzo maalumu kwa ajili ya kujifunzia kufyatua
matofali pamoja na jinsi ya kuendesha vikundi hivyo ili viwe vyenye
manufaa na endelevu
Pia alitoa wito halmashauri hizo kutumia vikundi vya vijana
hao kwa mahitaji ya matofali katika ujenzi mbalimbali, kwa lengo la kukuza
ajira kwenye maeneo yao na kuongeza kipato kwao ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kuwakwamua kiuchumi na kuondoka na umasikini.Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Home »
» Rukwa waaswa kuchangamkia fursa ya nyumba za NHC.
Rukwa waaswa kuchangamkia fursa ya nyumba za NHC.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment