Home » » UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma

UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Walter mguluchuma
Sumbawanga.

UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Kaimu Mkurugenzi wa hamashauri hiyo, Matrida Mwinuka alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya stadi za KKK yaliyowashirikisha walimu wa darasa la kwanza na pili wa shule 37 za wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa yaliyofanyika juzi kwenye ukumbi wa kituo cha walimu TRC kilichopo katika mji mdogo wa Matai wilayani humo.

Mwinuka alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha halmashauri hiyo inaondokana na idadi ya wanafunzi wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK) ambao mjongoni mwao wamekuwa wakihitimu elimu ya msingi kila mwaka.

"kimsingi tumejizatiti kuhakikisha tunawapa elimu ya stadi za kkk walimu wetu wanaofundisha wanafunzi wa darasa la saba ili kuhakikisha tunakuwa na wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wakijua kusoma, kuhesabu na kuandika hiyo ndio njia mojawapo ya kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) kupitia sekta ya elimu" alisema Mwinuka ambaye pia Ofisa elimu taaluma shule za msingi kwenye halmashauri hiyo.

Naye ofisa elimu taaluma shule za msingi Christina Bukori alisema kuwa hivi sasa idadi ya watoto wasiojua KKK waliopo darasa la saba ni 238 hivyo hali hiyo ndio imesababisha kufanyika kwa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo walimu hao ili waweze kuwafundisha watoto hao na wengineo na kuondokana kabisa na changamoto hiyo.

Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo, Ezekiel Lipingu alisema kuwa msingi mibaya ya kuwaandaa walimu katika vyuo husika ndio sababu ya ongezeko la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma kuhesabu na kuandika.

Alitaka kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuwaanda walimu katika vyuo hivyo ili watoke hapo wakiwa na stadi za kutosha za kumfanya mwalimu aweze kujua stadi hizo za kusoma, kuhesabu na kuandika.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa