Home » » SUMBAWANGA YAELEMEWA NA TAKA NGUMU

SUMBAWANGA YAELEMEWA NA TAKA NGUMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Sumbawanga imezidiwa na mzigo wa uzoaji wa taka ngumu kutoka eneo lililotengwa kwa ajili ya kukusanyia kutokana na uzalishaji wake kuwa mkubwa kuliko ilivyotarajiwa.
Hali hiyo imesababisha wakazi wa Kitongoji cha Sabato, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kukusanyia taka hizo, kuulalamikia uongozi wa manispaa  kwa kile walichodai kugeuzwa eneo hilo kama dampo la kudumu, hivyo kuhatarisha  afya zao.
Mmoja wa wakazi hao, Agness Chobalika, alisema pamoja na kufanya jitihada za kuwaeleza viongozi wa manispaa hiyo na mkoa juu ya kero hiyo ili kuliondoa dampo hilo, lakini hakuna aliyewajali.
“Tumeandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tukitaka waondoe dampo kwenye eneo hili, lakini hakuna aliyetujali zaidi ya kutupuuza,” alisema Agness.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela, alikiri kuzidiwa na uwezo wa kuzoa taka, kwani katika taka tani 70 zinazozalishwa, tani 28 ndizo zinazoweza kuzolewa na kwenda kutupwa kwenye dampo husika lililo nje kidogo ya mji huo.
Alisema sababu kubwa ya kushindwa kufanya hivyo ni ukosefu wa magari, kwani lililopo ni moja na limekuwa likishindwa kumudu wingi wa taka.
Chanzo:Tanzania Daima 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa