Home » » RAIS KIKWETE AMTEUA KAPT.CHILIGATI KUWA MWENYEKITI MKURABITA

RAIS KIKWETE AMTEUA KAPT.CHILIGATI KUWA MWENYEKITI MKURABITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amemteua kapteni John Chiligati kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara (Mkurabita) kwa kipindi cha miaka mitatu.
Sambamba na uteuzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, ameteua wajumbe 11 wa Kamati hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilisema kuwa walioteuliwa ni Ened Munthali ambaye ni Mratibu wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais Ikulu, John Nayopa, Kamishna Msaidizi wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Consolata Ishebabi, Mkurugenzi wa Wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs), Wizara ya Viwanda na Biashara na John Cheyo, Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha.

Wengine ni Profesa Aldo Lupala, Mkurugenzi wa Kituo cha Uchapishaji na Usambazaji, Chuo Kikuu cha Ardhi, Gasper Luanda, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Barke Mbaraka Aboud, Mkurugenzi Msaidizi wa Mikataba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeremia Sendoro, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI.

Wengine waliochaguliwa ni Parkshard Mkongwa, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu, Salhina Mwita Ameir, Mkurugenzi Mipango,

Sera na Utafiti, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Zanzibar, Mwita Mgeni Mwita na Kamishna wa bajeti, Wizara ya Fedha, Zanzibar.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa uteuzi huo umeanza Julai mosi, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa