Home » » MADIWANI WA WAMSUSIA KIKAO MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO BAADA YA KUKIUKA TARATIBU.

MADIWANI WA WAMSUSIA KIKAO MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO BAADA YA KUKIUKA TARATIBU.



 Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
Walter Mguluchuma , Sumbawanga.-RUKWA YETU
MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo iliyopo mkoani Rukwa, Philibert Ngaponda wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kugomea kuendelea kufanya na kikao cha baraza la madiwani kutokana na kile kinachodaiwa mkurugenzi huyo kukiuka kanuni na taratibu za uandaji wa mkutano mkuu wa baraza hilo.
Kwa mujibu wa madiwani wa Halmashauri hiyo, kabla ya kuitishwa mkutano mkuu wa baraza la madiwani mkurugenzi huyo alipaswa kuitisha kikao cha kamati ya fedha ili waweze kuijadili taarifa fedha kisha ndio ipelekwe kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani kitu ambacho hakikufanyika na mkutano huo kuitisha pasipo taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi juni.

Sakata la kugomea kikao hicho lilijitokeza muda mfupi mara baada ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Godfrey Sichona kufungua mkutano huo na mkurugenzi kusoma agenda ambazo zilipaswa kujadiliwa ndio madiwani wakiongozwa na Afred Mwanga walipokataa kuendelea na kikao hicho kwa madai ya kukosekana kwa taarifa ya fedha ya mwezi juni katika makabrasha waliyopewa.

Mwanga ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, kabla kuigawa na kuzaliwa kwa halmashauri ya Kalambo alihoji uhalali wa kufanyika kwa kikao hicho pasipo taarifa hiyo muhimu.

Hali hiyo ilisababisha mvutano kati ya madiwani na mkurugenzi ambaye alikuwa akiomba waendelee kikao hicho na kwamba taarifa hiyo itakuja kutolewa kwenye kikao kingine kitu ambacho wajumbe hawakukubaliana nacho kwa madai hata wajumbe ambao wangeijadili taarifa hiyo watakuwa wamebadilika kwa sababu kikao hicho kilipaswa pia kuchangua naibu mwenyekiti mwingine na kamati zake za kudumu.

Mvutano huo wa maneno baina ya Mkurugenzi na madiwani hao ulidumu kwa zaidi ya saa tatu tangu saa nne hadi nane kasorobo ndipo kikao hicho kipovunjika baada ya madiwani kushikiria msimamo wao wa kukataa kuendelea na kikao hadi kamati ya fedha ijadili taarifa ya mapato na matumzi ya mwezi juni ndipo ndio kiitishwe kikao kingine baraza la madiwani ambacho kitajadili taaifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na mapato na matumizi kwa mwaka uliopita.

"Sisi ni watu wazima na wengine tunauzoefu wa kutosha katika vikao hivi......huwezi kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pekee bila taarifa ya fedha, aache kutuburuza hapa na hatupo tayari kuvunja kanuni tuzojiwekea wenyewe kwa manufaa ya mtu mmoja....kulikuwa kuna usiri gani hapo wa kuficha taarifa ya fedha ya mwezi juni...."alihoji Leonard Shalamwana diwani wa kata ya Mwimbi.

Kutokana na mvutano huo, iliwalazimu madiwani hao kupiga kura ili kujua idadi ya madiwani ambao wako tayari kutoendelea na kikao ambapo madiwani wote kwa pamoja walinyoosha mikono kuashiria kukubali kikao hicho kivunjike.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatika zinadai kuwa awali baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo walimshauri mkurugenzi huyo asiitishe kikao cha baraza la masdiwani pasipo kuitisha kikao cha kamati ya fedha ili ijadili taarifa fedha ya mwezi juni lakini  haliwapuuza.

Awali mkutano huo mkuu wa baraza la madiwani ulipangwa kufanyika juni 28 mwaka huu lakini uliharishwa kutokana na ukosefu wa fedha hivyo kuzogezwa mbele  hadi juzi madiwani hao walipougomea kwa kukosekana kwa taarifa hiyo.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba madiwani hao na mkurugenzi huyo wamekuwa hawaelewani kwa kipindi kirefu sasa na walikuwa walitaka kamati ya fedha ijadili taarifa ya mapato na matumizi kisha ipeleke kwenye mkutano huo azimio la kumkataa mkurugenzi huyo kwa madai ya kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya fedha kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ambapo makusanyo yote ni sawa na asilimia 46 tu.

Hata hivyo wakati kamati fedha ikikosa fursa ya kujadili taarifa ya fedha, kuna taarifa zinadai kuwa kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa (RCC) kinachotarajiwa kufanyika mapema wiki hii halmashauri hiyo imewasilisha taarifa ya fedha inayoishia mwezi juni kitu ambacho kinashangaza wengi.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa