Home » » HOT NEWS: Polisi lawamani kwa kujihusisha na ujambazi Rukwa‏

HOT NEWS: Polisi lawamani kwa kujihusisha na ujambazi Rukwa‏


Na  Walter  Mguluchuma .
Sumbawanga

BAADHI ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao minadani mkoani Rukwa wamelitaka jeshi la polisi kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria askari wake wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.

Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutoandikwa gazetini, kwa nyakati tofauti mara baada ya kikao cha wafanyabiashara hao na mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kilichofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa, wafanyabiashara hao walidai kwamba matukio mengi ya uporaji wa kutumia silaha yamekuwa yakiwahusisha baadhi ya polisi wasio waaminifu ndani ya jeshi hilo.

Wafanyabiashara hao walisema kuwa mathalani tukio lilitokea juzi la magari zaidi ya matano yaliyokuwa yamewabeba wafanyabiashara wanaotoka mnadani tarafa ya Mtowisa kutekwa katika eneo la milima kizungu barabara ya Muze - Sumbawanga  na kuporwa vitu mbalimbali vya thamani yakiwemo mamilioni ya fedha wapo baadhi ya polisi walihusika na kutambilika.

"kwenye lile tukio kuna baadhi ya polisi wanahusika........tumewatambua kwa sura na majina na tumehaidi kutoa taarifa za siri kwa mkuu wa mkoa ili wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria, kwani wametufanyia vitendo vya udhalilishaji hasa dhidi ya wanawake......walikuwa wakiwapekuwa kama wana fedha hadi ndani ya nguo za ndani wengine kwa kuwa wanawafahamu wamepigwa sana......sasa hali hii haiwezi kuvumilika" alisema mmoja wao.

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Ferdinand Rwegasira alikiri kwamba yapo malalamiko ya wafanyabiashara dhidi ya baadhi askari polisi kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha lakini kama ilivyo taratibu wanapokea taarifa na kuzifanyia uchunguzi ili kuwabaini wahusika na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

"Kimsingi ni kwamba jeshi la polisi haliwezi kuvumilia ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wa amani.......sasa basi kama kuna mtu anafanya uhalifu awe polisi au raia yoyote yule tutamchukulia hatiua stahiki kwamwe hatuwezi kulifumbia macho uhalifu wa aina yoyote ile" alisema Rwegasira.

Awali, Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya, baada ya kupokea maombi ya wafanyabiashara hao wakitaka kupewa ulinzi wa polisi mara wanapoelekea kufanya shughuli zao minadani, alidai kuwa ombi hilo amelipokea hila kinachotakiwa kufanyika ni kutoa ratiba ya sehemu za minada yao ili polisi waweze kuwapatia ulinzi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa