Home » » UHARIBIFU MAZINGIRA ZIWA RUKWA WAHATARISHA ZIWA HILO KUTOWEKA

UHARIBIFU MAZINGIRA ZIWA RUKWA WAHATARISHA ZIWA HILO KUTOWEKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Ziwa Rukwa
Mustakabali wa wananchi wanaoendesha maisha kwa kutegemea rasilimali za ziwa Rukwa mkoani Rukwa uko shakani kufuatia uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi kukausha ziwa hilo.
Iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa Ziwa Rukwa litatoweka, imebainika.
Mhadhiri wa Idara ya Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Mshiriki, Hudson Nkotagu, alisema katika mahojiano na NIPASHE kuhusu hali ya ziwa hilo lililohatarini kutoweka.

Alieleza kuwa ziwa hilo ambalo karne zilizopita lilikuwa limeungana na Ziwa Tanganyika ( la Kigoma) linakauka kutokana na kilimo kisichozingatia utaalamu na ufugaji duni ambao unaingiza tope ndani ya ziwa hilo na pia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema ziwa hilo limepungua kina kutokana na kujaa tope ambao ni udongo unaosombwa na kuingizwa ziwani wakati wa mvua kutokana na mmomonyoko unaosababishwa na kilimo duni kisichokuwa na matuta wala makinga maji na ufugaji wa kizamani wa kundi kubwa unaolisha wanyama kiholela bila kujali kuwa wanamomonyoa ardhi na kuondoa uoto wa asili.

Profesa Nkotagu ambaye pia ni gwiji la elimu ya miamba na maji, alisema tope hilo limejaa kiasi kwamba hata kama mvua zinanyesha maji kidogo huiingia ziwani Rukwa na kukauka muda mfupi baada ya msimu kuisha.

Kwa upande wa uharibifu wa mazingira alitaja kuchoma mkaa, kukata kuni kuzalishaji mbao na kuchoma mapori kwa ajili ya kilimo kumeharibu uoto wa asili hivyo kupunguza mvua na kukausha vyanzo vingine vya maji vilivyokuwa vinaingiza maji ziwani.

Matokeo yake alisema ni pamoja na kupungua kwa samaki kunakoletwa na tope kufunika mazalia yake pamoja na mayai yao, tope kufunika na kuganda kwenye mapezi ya samaki hivyo kushindwa kupumua baada ya tope kuganda kwenye mapezi na samaki kushindwa kuelea kwenye maji yaliyojaa tope na takataka nyingine za kilimo.

Alisema panoja na uhaba wa kitoweo, inapunguza shughuli za uzalishaji na kuongeza umaskini hasa kwa wavuvi wanaondesha maisha yao kwa biashara ya samaki.

Akizungumzia athari za mabadiliko ya tabianchi alisema ongezeko la joto limesababisha maji kupotea kupitia mvuke. Athari za ukame na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu hivyo kukausha uoto wa asili na kuathiri akiba ya maji yanayoingia ziwani.

Profesa Nkotagu alisema ni kurudisha mazingira ya asili ya Ziwa Rukwa kwa kupanda miti na kulinda uoto wa asili akishauri kupanda nyasi (vetiva) zinazorudisha hali oevu ya ardhi.

Pia aliwashauri wananchi kuacha kilimo na ufugaji unaosababisha mmomonyoko na kujaza tope ziwani. 
CHANZO: NIPASHE
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa