Home » » BODA BODA AUAWA KWA KUCHINJWA, APORWA PIKIPIKI

BODA BODA AUAWA KWA KUCHINJWA, APORWA PIKIPIKI

Na   Walter   Mguluchuma 
Mpanda   Katavi
Mwendesha  Pikiipiki  (BODABODA) mmoja  anaefanyashughuli  zake   katika  kituo   cha  Hospitali  ya Wilaya  ya  Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  ameuwawa kiikatili   kwa  kuchinjwa na kukakatwa  na  mapanga   kisha kupolwa pikipiki  yake  na       mwili wake  kutupwa kichani

Kamanda  wa  jeshi  la Polisi  wa  Mkoa  wa  Katavi   Kamishana  msaidizi   mwandamizi    Dhahiri   Kidavashari  alimtaja  Bodaboda  aliyeuwawa kwa kuchinjwa  kuwa  ni Samweli  Joseph  Vitalisi  (31) Mkazi  wa  Mtaa  wa Nsemlwa    mjini    Mpanda
Kwa mujibu  wa  Kamanda   Kidavashari  tukio  hilo la  mauwaji ya  kusikitisha  lilitokea  hapo juzi  majira ya saa kumi  jioni   katika   eneo  la   Kijiji  cha  Mpembe  Kata ya Katuma   Tarafa ya  Mwese  Wilayani   Hapa
Alisema  siku  hiyo ya  tukio  marehemu  akiwa  kwenye   kituo  chake   cha  kufanyia   shughuli   hapo majira ya  saa  tisa  alasiri  akiwa na  Bodaboda  wenzake  alitokea  mteja mmoja  ambae  alimwomba  marehemu  wafanye   nae  mazungumzo ya  maelewano ya  kiwango cha  bei  ya  kumsafirisha  kwa  kutumia  pikipiki yake  aina ya SUN LG   yenye   namba  za usajiri   T 704  CDQ kwa lengo la kumpeleka   katika  kijjii  cha  Mpembe  kilichoko  umbali wa kilometa  72 kutoka   Mjini  Mpanda
Alisema   katika  maongezi yake abiria  huyo alimweleza   mwendesha pikipi   BODABODA  kuwa  anahitaji usafiri huo  iliaweze  kwenda  kijijini  kuchukua  fedha kwa  ndugu  zake  kwa  ajiri ya kukodi gari  la   kkusafirishia  mweli wa  marehemu   ndugu  yake ambae  mwili wake  ulikuwaumehifadhiwa katika   chumba  cha  kuhifadhi maiti  katika  Hospitali ya Wilaya  ya Mpanda  ili aweze  kuusafirisha kwenda kwenye Kijiji  hicho cha Mpembe kwa ajiri ya  mazishi
Kamanda  Kidashari  alieleza   baada ya  makubaliano  baina  yao  kati ya Bodaboda  na  mteja wake walikubaliana kuanza  safari ya kwenda  kijijini  huko  licha ya Bodaboda  wenzake   kumtaka umarehemu awaeleza mahari ambako  anampeleka mteja huyo  lakini marehemu hakuwa wazi kuwaeleza mahari anakoelekea kwa kuhofia wenzake wanaweza  kumshawishi mteja wake  achukue   bodaboda mwingine
 Alisema  baada ya marehemu kuondoka  hapo juzi  hakuweza kuonekana tena kwenye kituo chake cha kazi hadi hapo jana ambapo  badaboda wenzake walipopata   mashaka ya kutoonekana  mwenzao  toka alipoondoka  na mteja wake na ndipo walipotowa taarifa kwa jeshi la polisi ambao  nao waliwasiliana  na uongozi wa kijiji hicho juu ya kutoweka kwa marehemu  
Kamanda Kidavashari   alisema  ndipo hapo jana  majira ya saa saba  mchana  mwili wa marehemu ulipookotwa ukiwa  kwenye kichaka katika kijiji hicho  cha Mpembe huku ukiwa umechinjwa shingo na kukatwa kwa panga kichwani na mkononi na pikipiki yake ikiwa imepolwa

Jeshi la polisi  Mkoa wa Katavi limetowa wito kwa  waendesha  pikipiki   bodaboda kuacha tabia ya kuwachukua abilia ambao wasio wafahamu na kusafiri nao  umbali mrefu hasa kwenye maeneo ya nje ya mjin na jeshi hilo bado linaendelea na msaka wa kuwatafuta na kumtafuta  mtu awa watu waliohusika na mauwaji hayo kwani mpaka sasa hakuna mtu alikamaatwa  kuhusiana na tukio hilo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa