Home » » WAZIRI WA AFYA ALALAMIKIA WANAOHUJUMU VIFAA VYA TIBA

WAZIRI WA AFYA ALALAMIKIA WANAOHUJUMU VIFAA VYA TIBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Afya Dk. Seif Rashid amesema huduma za afya hapa nchini zimekuwa zikidorora kutokana na baadhi ya wahudumu wa afya kutumia vibaya vifaa tiba vilivyopo kwenye maeneo yao ya kazi.

Waziri huyo wa afya ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua kituo cha upasuaji cha Mtowisa kilichopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ambacho kimejengwa na mashirika matatu ya kimataifa yaliyoungana katika kutoa huduma ya afya Uzazi na Mwana.

Akizungumza na wananchi wa tarafa hiyo Dk. Rashid amesema pamoja na serikali kujitahidi kuboresha huduma za afya hapa nchini bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za kiutendaji na bajeti ya kutosha.

Amesema wahudumu wa afya wanatakiwa kuwa waadilifu katika vituo vyao vya kazi kwani wapo baadhi yao ambao hata vifaa tiba vinavyotolewa kwenye maeneo yao wamekuwa wanavitumia ovyo na kuhariribika kwa haraka lakini baadhi pia wamekuwa wakituhumiwa kuvihamisha vifaa hivyo na kupeleka kwenye sehemu sizizo kusudiwa hivyo kufifisha mikakati ya serikali ya kuiboresha huduma za afya.

Amewataka wahudumu wa afya kutumia muda wao na taaluma walizonazo katika kutoa huduma zilizobora kwa wananchi kama yalivyo malengo ya serikali katika kutoa huduma bora za afya.

Aidha Dk. Rashid ameyapongeza mashirika ya Africare, Plan International na Jphgo kwa ushirikiano wao kwa kuhakikisha huduma za afya kwa akinamama wajawazito na watoto wachanga zinapatikana katika mkoa wa Rukwa, kwa kuamua kujenga vya upasuaji vya Mtowisa wilayani Sumbawanga na Wampembe wilayani Nkasi.

Amesema maeneo hayo na mengineyo nchini yamekuwa tatizo la upatikanaji kwa huduma za haraka za upasuaji hivyo kupoteza uhai wa wanawake na watoto wengi.

Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mwana Gwynneth Wong amesema shirika hilo linajitahidi kuweka mikakati ya kupunguza baadhi ya changamoto katika maeneo ya mradi huo ikiwa ni pamoja kujenga vituo vya upasuaji sanjari na kutoa magari ya wagonjwa ili kuokoa uhai wa akinamama wajazito na watoto wachanga.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa