Home » » SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UUZWAJI WA DAMU HOSPITALINI‏

SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UUZWAJI WA DAMU HOSPITALINI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Walter Mguluchuma,
Sumbawanga.

SERIKALI imetakiwa kuchukua hatua za makusudi kudhibiti biashara ya uuzwaji wa damu inayofanywa wataalamu wa afya wasio waaminifu kwenye vituo vya umma vinavyotoa huduma ya afya hapa nchini.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Evidence for Action Tanzania Craig John, inayoendesha kampeni ya mama ye! alisema hayo wakati akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utepe Mweupe yanayokwenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa hiari wa damu kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambayo yaliyofanyika katika miji wa Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa.


John alisema kwamba imebainika kwamba baadhi ya vituo vinavyotoa huduma ya afya hususani wilaya hospitali za wilaya nchini,biashara ya uuzwaji wa damu ambayo wananchi wamechangia imeshamiri na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kudhibiti hali hiyo kitu ambacho kinasababisha ongezeko la vifo vya wakinamama wajawazito kabla, wakati na baada ya kujifungua.


"Lazima Serikali ishiriki kikamilifu katika kampeni ya kuokoa maisha ya wajawazito kwa kudhiti tabia ya baadhi ya wataalamu wa afya ya kuuza damu kwa wagonjwa hususani wakina mama wajawazito wanaofikishwa hospitali kwa ajili ya kujifungua kwa upasuaji kwa ni ndio chachu pia ongezeko la vifo katika hospitali zetu" alisema John.


Mkurugenzi wa Evidence for Action Tanzania alisema kuwa pamoja na kwamba ni kosa kwa kuuza damu kama ambavyo sera ya afya inavyoeleza damu itolewe bure lakini pia kutokana na baadhi ya wananchi kugundua kwamba kuna biashara hiyo inafanyika kinyume na utaratibu mwamko wa wananchi kuchangia damu umekuwa mdogo ukilinganisha na miaka ya nyuma.


Aliongeza kuwa pia ipo haja kwa Serikali kutenga bajeti maalumu ya fedha za kutosha za kuhakikisha uwepo wa huduma za dharula za kumuokoa mjamzito na mtoto mchanga wakati wa kujifungua katika kila kituo kinachotoa huduma za afya kwani ni chachu ya kupunguza kwa asilimia 75 vifo vya wajawazito na watoto wachanga.


Inaelezwa kwamba kituo chenye kutoa huduma za dharula (CEmONC) kinatakiwa kuwa na wodi ya wazazi yenye kutoa huduma kwa ufanisi, ikiwemo chumba cha kujifungulia, chumba cha upasuaji na benki ya damu ili akinamama wanaohitaji, waweze kujifungua kwa njia ya upasuaji na kuongezewa damu.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa