Home » » Msigallah: Mjadala usiwe wa Muungano pekee

Msigallah: Mjadala usiwe wa Muungano pekee

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Fredrick Msigallah amewataka wajumbe wenzake kuacha kujikita katika kujadili masuala ya muundo wa Muungano pekee katika mchakato wa kutunga Katiba mpya.
Msigallah, ambaye anatoka kundi la walemavu, alisema kwa bahati mbaya sasa mjadala wa katiba umetekwa na wanasiasa, ambao wanatumia muda mwingi kujadili mambo ya Muungano pekee.
“Kwenye Rasimu ya (Tume ya) Jaji Warioba ametuandikia mambo mengi sana tena ni muhimu kwa maelezo ya taifa letu, lakini tatizo ambalo naliona sasa ni wengi kujikita katika mambo ya Muungano,” alisema Msigallah.
Alifafanua kuwa kundi la walemavu, linaifurahia rasimu hiyo kwa kuwa imetambua haki zao, lakini, wanaamini bado kuna haki ambazo wangetaka ziingizwe kwenye katiba mpya.
“Tunataka haki ya kupata elimu bure, kwani kati ya watoto 100 wenye walemavu ni watoto kumi tu ndio wanaweza kupatiwa elimu,” alisema Msigallah.
Alisema pia wanataka haki ya kupata huduma nyingine muhimu ikiwamo huduma za afya kuwa bure na mahitaji maalumu, ikiwamo wenye udhifu wa kuona kuwezeshwa kupata vifaa vya kuona vizuri, walemavu wa macho wawezeshwe kupata elimu kupitia nukta nundu na chombo cha kutetea na kulinda haki za walemavu.
Hata hivyo, alisema anaamini kadri siku zinavyosonga, wajumbe watarejea kwenye mchakato wa Katiba na kuanza kujadili rasimu katika mambo ambayo ndio kilio cha wananchi hasa wa vijijini.
Chanzo;Mwananchi
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa