Home » » WAAJILI NCHINI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUWASHIKIZA WAAJILIWA‏

WAAJILI NCHINI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUWASHIKIZA WAAJILIWA‏

Na Walter Mguluchuma-Rukwa yetu Blog
Sumbawanga.

WAAJIRI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwashikiza waajiriwa wapya Serikalini na kwenye taasisi mbalimbali kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii ya kujiunga nayo na badala yake wawache wachague wenyewe mifuko sahihi ambayo itakuwa na manufaa kwao kabla na baada ya kustaafu.

Meneja uendeshaji wa mfuko wa Pensheni wa LAPF, Victor Kikoti alisema hayo jana wakati akitoa semina ya kuhusu faida ya kujiunga na mfuko huo, kwa wanachuo wa chuo cha madaktari wasaidizi kilichopo mjini hapa.

Alisema kuwa tabia ya waajiri kuwashikiza waajiri wapya kujiunga na baadhi ya mifuko ya jamii ambayo wao wamejiunga nayo imekuwa kisababisha waajiri hao kutofanya chaguzi sahihi hivyo kupata usumbufu haki zao wanazostahili kuzipata kabla na baada ya kustaafu.

 "kwa kuzingatia uhuru uliopo hivi sasa wa waajiriwa wapya wasishinikizwe kujiunga na mfuko ambao baadhi ya waajiri (maofisa utumishi) wamejiunga......kwani wapo waliokosea njia na kujiunga na mifuko ambayo imepoteza uelekeo na ina usumbufu mkubwa kwa wateja wake hivyo si vema hawa nao wakashinikizwa bali ni kuwasaidia kupata ufahamu wa mifuko ambayo itakuwa na manufaa kwao" Alisema Kikoti.

Aliongeza kuwa pia changamoto kubwa ambayo wamebaini inawakabili waajiriwa wapya ni pamoja na kutojua kama uzee na ufahamu mdogo kuhusu mifuko bora ambayo inalipa kwa haraka mara baada ya mtumishi kustaafu.

Alisema kuwa LAPF imejikita kuwahamasisha wahitimu wa fani hiyo ya uuguzi kuhusu mafao mbalimbali yanayotolewa na mifuko ya jamii yanalenga kuwawezesha watumishi kukabilina na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa