Home » » MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MKOANI RUKWA

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MKOANI RUKWA

 Mkazi mmoja wa kitongoji cha Jangwani mjini Sumbawanga akihama kwa kutumia mkokoteni kutoka eneo moja kuelekea jingine kama alivyonaswa na mpiga picha wetu. Picha na Mussa Mwangoka.

 Baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kama boda doda wakiwa katika foleni ya kusubiri mafuta katika kituo kimoja kinachouza bidhaa hiyo, mafuta aina ya petroli yameadimika mjini Sumbawanga baada ya juzi mamlaka ya kudhibiti bei ya nishati na maji kutangaza kushuka kwa bei ya mafuta kutoka Sh 2500 hadi 2100. Picha na Mussa Mwangoka.
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Land Cruser jana wakifanya safari kati ya Sumbawanga mjini kuelekea Bonde la Ziwa Rukwa, hali hiyo ni hatari kwa watu na mizigo lakini inajitokeza kutokana na ugumu wa usafiri katika maeneo hayo. Picha na Mussa Mwangoka.
Blogzamikoa

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa