Home » » Joketi Miss Rukwa mpya

Joketi Miss Rukwa mpya


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa yetu

JOKETI Joseph (20) ameibuka kuwa mrembo wa mkoa wa Rukwa (Redd’s miss Rukwa 2012) katika mashindano yaliyofanyika jana usiku katika  ukumbi wa Bomani uliopo mjini Sumbawanga.

Joketi ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa, aliwashinda washiriki wenzake tisa kwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang’anyiro kilichojaa ushindani wa kila aina.

Jaji mkuu wa shindano hilo, Ismail Mpagama, alimtangaza mrembo huyo kuwa mshindi wa kwanza,  nafasi ya pili ikienda Asia Abdalah (19)  na mshindi wa tatu alikuwa Vency Edward (18).

Hata hivyo katika shindano hilo, ilionekana dhairi  kwamba Joketi ataibuka na ushindi kwani alikonga nyoyo za watu waliojitokeza ambapo kila alipopita jukwaani alishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kwenye ukumbi huo .

Kwa mujibu wa muandaaji wa shindano hilo, Mariam Amri mshindi wa kwanza ajipatia zawadi ya Seti moja ya Tv na dish kutoka kampuni ya Zuku sambamba fedha taslimu Sh 300,000, mshindi wa pili akijivunia Sh 200,000 na watatu akiweka kibindoni Sh 170,000 washindi wa nne na tano walijipatia Sh 120,000 kila mmoja huku washiriki wengine watano  wakiambulia kifuta jasho cha Sh 100,000.

Muandaaji huyo aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kusaidia kufanikisha mashindano hayo huku akiahidi kuwa washindi hao watawakilisha vema katika mashindano yajayo ya kanda ya nyanda za juu kusini na yale ya  Redd’s miss Tanzania 2012 ngazi taifa.

Baada ya kuibuka na ushindi Joketi alisema kuwa atajitahidi kadri awezavyo kuibuka na ushindi katika mashindano ya kanda na kupata tiketi ya kuingia katika ngazi ya kitaifa ambako nako ametamba kushinda na taji hilo kwenda Rukwa safari hii.

Mwisho.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa